Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Uchaguzi wa Udiwani Kata nne za Arusha kufanyika Juni 30, 2013

Dar es Salaam.

Tume ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kurudiwa kwa uchaguzi mdogo katika kata nne za Arusha ambazo ni Kimandolu, Elerai, Themi na Kaloleni ambazo zilisimamishwa kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa madiwani kutokana na vurugu zilizojitokeza katika kampeni za mwisho za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na sasa utafanyika Juni 30 mwaka huu.

Mkurugenzi wa NEC,Julius Malaba alisema jana Dar es Salaam kuwa kutokana na hali hiyo, wananchi wa eneo hilo wanapaswa kwenda kwenye vituo vya kupigia kura,ili waweze kuhakiki majina yao ili kuondoa usumbufu siku ya kupiga kura.Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo wananchi wa eneo hilo wametakiwa kutulia kwenye makazi yao mpaka uchaguzi utakapofanyika tena.

Malaba alisema ikiwa NEC imetangaza kusimamisha uchaguzi katika maeneo yoyote nchini, wanasiasa wanapaswa kuacha kufanya kampeni mpaka uchaguzi utakaporudiwa tena, na kwamba ikiwa baadhi ya vyama vitabainika kwenda kinyume na sheria hiyo vitafikishwa kwenye kamati ya maadili kwa sababu watakuwa wamevunja sheria za uchaguzi.

Alisema, kutokana na hali hiyo,wananchi wanapaswa kuwa makini katika kipindi hiki na kuhakikisha kuwa hawashiriki kwenye mikutano ya kampeni inayofanyika maeneo yao ili kuondoa migogoro ambayo inaweza kujitokeza.

Imeandikwa na Mwananchi

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO