Wabunge wa Chadema, Mh Lema, Mh John Mnyika, Mh Mashishanga, Mh Tundu Lissu na Grace Kiwhelu wakiwa wamebeba jenenza leneye mwili wa marehemu Judith William Moshi kuelekea makaburi ya Sokoni 1 kwa maziko. Marehemu Judith alifikwa na mauti baada ya kulipukiwa na bomu siku ya Mkutano wa Chadema kuhitimisha kampeni zake kwa udiwani wa Kata ya Kaloleni, mkutano uliofanyika uwanja wa Soweto siku ya Jumamosi Juni 15, 2013. Wabunge wengi wa Chadema walishiriki ibada na kuhudhuria mazishi wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho taifa Mh Freeman Mbowe.
Misa katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Usharika wa Sokon 1
Msafara wa kwenda Makaburini ukiongozwa na Askofu Isaac Kasir katka Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Usharika wa Sokoni 1
Baadhi ya wabunge wa Chadema wakiwa na huzuni eneo la makaburi
Jeneza likiteremshwa kaburini
Mh Freeman Mbowe na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi “Sugu” wakiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu
Mtoto wa marehemu akilia kwa uchungu sana baada ya kuweka shada la maua. Marehemu Judith ameacha watoto watatu wote wa kike
Msafara wa wafuasi wa Chadema ukitoka Hospitali ya Mt Meru kuelekea Kata ya Sokoni 1 ambako ndipo misa ya kumuombea marehemu na maziko ya Judith Moshi aliyekufa kwakulipuliwa na bomu Jumamosi iliyopita ilifanyika
Msafara ukikatiaza mitaa ya Jiji kiasi cha kusimamisha shughuli zote katika njia ilikopitia
Mbunge wa Ubungo, Mh John Mnyika akisalimiana na wachungaji baada ya mazishi
Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema na mkewe wakienda kuweka shada la maua
Wabunge kina mama nao wakiweka mashada ya maua
Wananchi wa kawaida nao wakishiriki kuweka mashada ya maua
Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni Mh Tundu Lissu akiweka shada la maua
Viongozi wa Chadema Mkoa wa Arusha
Viongozi wa Chadema Wilaya. Picha zote na Tumainiel Seria
Hapa ni Sugu akiwa na Peter Msigwa wakiongoza msafara.
Hili ndilo jeneza lililolobeba mwili wa marehemu ukipelekwa Sokon 1
Vijana walioko kwenye mafunzo ya upolisi wakiwa juu ya kanisa linaloendelea kujengwa wakati wa ibada ya kumuombea marehemu Judith William Moshi. Chadema inawatuhumu Polisi ndio waliolipua bomu na kupiga risasi zilizoua 4 na kujeruhi zaidi ya 67 katika mkutano wake
0 maoni:
Post a Comment