Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Hali halisi ya Soweto leo… Magari ya Matangazo ya Chadema yalitolewa upepo na risasi kwenye vurumai ya mabomu jana ; yasombwa na Polisi.

DSC09404Gari ambalo hutumika akama jukwaa la matangazo kwa mikutano ya Chadema (PA 12) ikikokotwa kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha asubuhi ya leo baada ya kuachwa hapo na dereva wake jana wakati wa vurumai ya Polisi kuwashambulia wafuasi wa Chadema kwa mabomu ya machozi na risasi za moto kuwaondoa katika viwanja vya Soweto Jijini hapa ambapo muda huo walikuwa wakisikiliza maelezo ya viongozi wao.

DSC09414Baadhi ya baiskeli maalumu za kuuzia ice ream za Azam zikiwa zimerundikwa eneo moja na viti vilivyokuwa vikitarajiwa kutumiwa na wageni waalikwa kwa shughuli ya kuaga miili ya marehemu waliokufa kwa kulipuliwa na bomu ama risasi.

DSC09406Gari ya Chadema ikitembezwa huku matariri mawili yakiwa hayana upepo. tairi hizi zilitoolewa na risasi jana jioni ili kutoziwezesha kuondosha gari hiyo.

DSC09409

DSC09412

DSC09407

Hali halisi asubuhi ya leo katika viwanja vya Soweto. Hakuna askari wanaolinda kama ilivyokuwa jana. Eneo la mlipuko bado limezungushiwa uzio wa hatari. Wananchi walitembelea tena eneo hilo mapema asubuhi kama wanavyoonekana pichani.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO