Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Tume ya Uchaguzi yaahirisha tena Uchaguzi wa Madiwani Kata nne za Arusha hadi 14 Julai 2013

DSC07392Mwenyekiti wa Chadema ambae pia nai Mbunge wa Hai na Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni, Mh Freeman  Mbowe akishangaa umati wa watu katika mkutano wa Chadema kufunga kampeni zao uliofanyika Jumamosi ya Juni 15, 2013 uwanja wa Soweto Jijini Arusha na kuishia kwa watu wanne kuuwawa na zaidi ya 70 kujeruhiwa na bomu na risasi zilizozuka katika mkutano huo. Miongoni mwa waliofariki alikuwamo pia Katibu wa Chadema Kata ya Sokoni 1. Majeruhi ambao bado hali zao ni mbaya ni pamoja na Katibu wa Lema, Gabriel Kivuyo na Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Sombetini Bw Madava ambao bado wanavyuma mwilini. Wengine ni walinzi wa chama hicho na wananchi wengine.


Tume ya Uchaguzi ya Taifa imetangaza kuahirisha uchaguzi mdogo wa Madiwani uliokuwa ufanyike tarehe 30.06.2013 katika Kata nne -Elerai, Themi, Kaloleni, Kimandolu- za halmashauri ya Manispaa ya Arusha.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema badala yake uchaguzi huo utafanyika tarehe 14 Julai 2013.

Amesema sababu kubwa ya kuahirisha tena uchaguzi huo ni kuwapa wananchi muda wa wiki mbili zaidi za kutulia kutokana na taharuki iliyotokea katika mkoa huo siku chache zilizopita, hali ambayo inaweza kuathiri upigaji kura na matokeo.

Uchaguzi huo awali ulipangwa ufanyike Jumapili ya terehe 16 Juni 2013, lakini uliahirishwa baada ya kutokea shambulio na mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa mwisho wa kampeni za CHADEMA, siku ya Jumamosi ya tarehe 15 Juni 2013, shambulio ambalo lilisababisha vifo vya watu wawili papo hapo na wengine wawili siku chache baadaye.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO