Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mwigulu Nchemba, Peter Msigwa nusura watwangane makonde Dodoma jana

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba jana nusura wachapane makonde baada ya kutupiana maneno ya kashfa, wakituhumiana kuhusika na mlipuko wa bomu uliotokea Jumamosi iliyopita mkoani Arusha.

Tukio hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji wa Dodoma, walipohudhuria semina ya wabunge wapambanaji na UKIMWI, ambapo baadhi ya wabunge wa CHADEMA walihudhuria.

Malumbano hayo yanatokana na Nchemba kuituhumu CHADEMA kuhusika na mlipuko wa bomu huko Soweto, Arusha (kwenye mkutano wao wa kufunga kampeni za Uchaguzi wa Madiwani katika Kata za mkoa huo, siku ya Jumamosi ya Juni 25, 2013), Juni 20 mwaka huu wakati akichangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2013/2014, akisema chama hicho kilipanga kulipua bomu hilo ili kuwafanya Watanzania waamini kuwa Serikali ya CCM ndiyo inayohusika na tukio hilo.

Msigwa akiingia katika ukumbi huo akiwa ameongozana na Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA), Ezekiah Wenje, walikutana uso kwa uso na Nchemba ambaye alikuwa akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Said Amour Arfi. Baada ya Nchemba kumwona Msigwa alimkaribisha mchungaji huyo akisema;

Karibu sana bwana, salama lakini?”

Hata hivyo, badala ya kujibu salamu hiyo ya Nchemba, Msigwa alikuja juu na kumtuhumu Nchemba kwamba anatoa kauli zinazoweza kuvuruga amani ya nchi: “Wewe ni mtu hatari sana, haya yote yanasababishwa na wewe, mnatumia damu za watu kutafuta madaraka,” alisema Msigwa akimtupia maneno Mwigulu.

Baada ya kauli hiyo Nchemba alihoji akisema: “Ki-vipi? Hayo mambo tuyaache, Msigwa achana na haya mambo!

Baada ya Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM kujibu, Msigwa alimsogelea karibu na kumnyooshea kidole, huku akiendelea kumtuhumu kuwa ana siasa chafu zinazopandikiza chuki kwa jamii.

Malumbano hayo pia yaliingiliwa na Mbunge wa Musoma Mjini (CHADEMA), Vicent Nyerere ambaye alimuunga mkono Msigwa, huku akimtuhumu Nchemba kuwa ni mtu mbaya katika siasa za Tanzania.

Katika kile kilichoonekana kutaka kuweka mambo sawa, Wenje alimvuta Msigwa na kumpeleka ukumbini ili kuepusha shari baada ya wabunge hao kuzidi kurushiana maneno. Hata walipoingia ndani ya ukumbi huo wabunge hao waliendelea kulumbana, lakini wakatulizwa na baadhi ya wabunge waliokuwa karibu yao.

Alipotakiwa kueleza sababu za mzozo huo na Nchemba, Mchungaji Msigwa alisema, “Achana na yule mpuuzi, mimi siwezi kuzungumza na mtu mnafiki, mkatili na yeye ndiye alihusika na mipango mibaya dhidi ya CHADEMA hata mlipuko wa Arusha hivyo kutesa watu wa CHADEMA.”

Alisema kuwa yeye haoni sababu ya mtu mwenye mipango mibaya na wananchi wa Tanzania pamoja na chama chake (CHADEMA), kuwafuata na kujikomba.

Kwa upande wake Nchemba alipoulizwa alisema kuwa alichokizungumza ni mtazamo wake na kwamba ikiwa kuna mtu anayeona kuwa alizungumza uzushi, ajitokeze na kupinga: “Nilichokizungumza ndicho kilichofanyika kwa matukio yote niliyoeleza bungeni,”alisisitiza Nchemba.

Chanzo: Chadema Blog

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO