Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Green Guard wa CCM watuhumiwa kujaribu kuvuruga mkutano wa Chadema Kata ya Themi Arusha kwa silaha kali, mmoja akamatwa na kufikishwa Polisi

DSC07095Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba za viongozi wa Chadema (hawaonekani pichani) katika mkutano wa Chadema eneo la Ekenya, Kata ya Kaloleni Mei 30, 2013. Picha hii haina uhusiano na mkutano uliofanyika Themi jana na kunusurika kuvurugika.

Taarifa ambazo Blog hii imezipata na kuthibitishwa na Jeshi la polisi zinaeleza kuwa siku ya jana eneo la
Kambarage – Themi kulikuwa na tafrani katika mkutano wa Chadema waa kumnadi mgombea wa chama hicho katika Kata hiyo baada ya vijana waliogundulika kujaribu kutaka kuvuruga mkutano huo.
Vijana hao ambao mmoja wao Joseph Laiser alikamatwa eneo la mkutano  akiwa ameficha shoka na kisu ndani ya koti lake na kufikishwa kituo kikuu cha Polisi Arusha jioni ya jana na kufunguliwa kesi ya Kutishia kwa Shoka na Kisu ikiwa imesajiliwa kwa RB No. AR/RB/6937/2013
Joseph Laiser anadaiwa aligunduliwa na walinzi wa Chadema waliomtilia mshaka na kumfuatilia nyendo zake na kunasa mawasiliano yake akiwaita vijana wengine waliotambulishwa kwa majina maarufu kama Jumanne Mjusi na Mojaa ambao hawakukamatwa.
Katika ufuatiliaji sakata hilo, Katibu wa Uchumi Wilaya Arusha Mjini, Victor Mollel alifika Kituo kikuu cha Polisi Arusha kumwekea dhamana
Joseph Laiser lakini akaishia kuswekwa rumande kituoni hapo baada ya kumtishia mmoja wa viongozi wa Chadema kituoni hapo mbele ya askari polisi kwa bastola yake, na akafunguliwa jalada kwa RB No. AR/RB/6938?2013 - kosa la Kutishia kwa Bastola.

Aliyeandika maelezo kwa upande wa Chadema ni Bw Calist Bush ambaye ni Meneja kampeni wa mgombea wa Chadema kata ya Themi na alikuwa mkutanoni hapo akishuhudia matukio yote na ndieye anyeelezwa kuwataarifu polisi kufika mkutanoni hapo kusaidia usalama.

Aidha, ilielezwa pia kwamba kuna kijana mwingine ambae Blog hii haijapata jina lake alikamatwa na walinzi wa Chadema katika mkutano huo akisursha mawe lakini Mbunge wa Arusha Mjini aliyekuwa akihutubia alimpandisha jukwaani na kuombewa masamaha, akaachiwa.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO