Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mbowe atembelea eneo la Mlipuko , Afariji wafiwa na Kujulia hali majeruhi wa shambulio la bomu katika Mkutano wa Chadema jana.

DSC09341Mwenyekiti wa Chadema, Mh freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema wakiwa katika uwanja wa Soweto mchana wa leo wakati zoezi la kuchukua vipimo mbalimbali likiendelea chini ya usimamizi wa wataalamu toka Jeshini.

DSC09327

Mbowe na Lema wakishauriana jambo..

DSC09343Eneo la maafa. Inaelezwa kuwa wataalamu wa jeshi waligundua kuwako kwa kitu ndani ya tanki la mafuta na hivyo kuamua kulikata. Taarifa hizo zinadai kwamba kulikuwa na mabomu yametegwa chini ya gari na hivyo tank hilo lilishmabuliwa kwa risasi labda utokee mlipuko! Pia gari hii ya amatangazo ina majeraha mawili mlango wa kushoto yaliyotokana na kitu chenye ncha mabacho kinaweza kuwa risasi au vipande vya vyuma vya bomu.

DSC07458

DSC09360Mh Mbowe akiwa nyumbani kwa wazazi wa mmoja wa marehemu (Ramadhani) eneo la Mianzini kuwapa pole kwa kuondokewa na mpendwa wao.

DSC09382James Ole Millya na Mbunge Lema wakimjulia hali mmoja wa majeruhi walilazwa hospitali ya Seliani

DSC09373Mtoto Sharifa nae amalazwa hospitalini hapo kwa majeraha ya mlipuko

DSC09377Dereva wa mgombea wa Chadema Kata ya Themi, Bw beni akiwa majeruhi kitandani

 

IMG-20130616-WA0006

Kamanda wa Chadema ambaye alikuwa ni mlinzi wa amani (Red Brigade) katika mkutano huo, Bw Kitumbwizi akiugulia maumivu katika hospitali ya Selian alikolazwa baada ya kujeruhiwa katika mlipuko huo. Huyu amaumizwa mguu mmoja, mkononi na sehemu ya kwapani ambapo imegundulika kuwa kuna chuma ama risasi ndani ambayo imekuwa ngumu kutolewa mapaka sasa.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO