Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CCM, Chadema wakatana shoka Kameni za Udiwani Arusha

Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema akimwangalia Amos Ibrahim ambaye amejeruhiwa kwa kukatwa na shoka wakati akitibiwa katika Hospitali ya Mount Meru. Picha na Mussa Juma


 Arusha.

Siku chache baada ya mtu mmoja kujeruhiwa sehemu ya jicho katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani jijini Arusha, mtu mwingine amevamiwa na kukatwa na shoka mdongoni.

Aliyekatwa shoka ni Amos Ibrahim mfuasi wa Chadema, ambaye hadi jana, alikuwa amelazwa katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru. Mtu wa kwanza kujeruhiwa katika kampeni hizo ni Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Kata ya Engutoto, Joseph Laizer aliyejeruhiwa akiwa katika Kata ya Themi.

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa, akizungumza na Mwananchi alisema Ibrahim alivamiwa usiku wa kuamkia leo.

“Kijana huyu, alivamiwa na vijana wa CCM waliokuwa wanapiga kampeni za nyumba kwa nyumba usiku na walipofika kwenye chumba chake eneo la majengo alisema yeye ni Chadema na hivyo hatawapa kura na ndipo walimpiga,” alisema Golugwa.

“Baada ya tukio hili, tulitoa taarifa polisi tukapewa RB namba AR/RB/7134/2013 na tukapewa hati ya matibabu lakini wahusika hawajakamatwa” alisema Golugwa.

Alisema kutokana na vurugu ambazo sasa zimeanza kushamiri, wafuasi wa Chadema watakuwa wakijilinda wenyewe na watawakamata watuhumiwa na kuwashughulikia na baadaye ndiyo watapelekwa Polisi.

“Tutawakamata watuhumiwa, tutawashughulikia na baadaye ndiyo tutawapeleka Polisi” alisema Golugwa.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha, Dk Wilfred Soileli alikana kuwa wafuasi wa CCM kutenda kosa hilo na kueleza vijana wa Chadema ndiyo wamekuwa wakifanya uvamizi.

“Sisi hatuna taarifa za vijana wetu kufanya uhalifu huo, ila sisi ndiyo tumekuwa tukipigwa na kuzomewa mara kwa mara na vijana wa Chadema,” alisema Dk Soileli.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema, jeshi hilo linafanya uchunguzi wa matukio ya vurugu na wahusika watakamatwa.

“Tunataka kampeni ziwe za amani na utulivu, sasa kama kuna wakorofi hatua za kisheria zitachukuliwa tu” alisema Kamanda Sabas.

Uchaguzi wa udiwani wa kata nne za Kaloleni, Themi, Kimandolu na Elerai, utafanyika Juni 16 mwaka huu, baada ya waliokuwa madiwani kufukuzwa uanachama na Chadema.

Chanzo: Mwananchi

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO