Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Maalim Seif awataka wakazi wa Arusha kuitunza amani

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka wakazi wa Arusha kuilinda na kuitunza amani iliyopo ili kuuendeleza mji huo kiuchumi.

Maalim Seif alitoa wito huo katika kata za Themi na Kaloleni mjini Arusha, wakati akiwahutubia wakazi wa maeneo hayo kwenye mikutano ya kampeni za udiwani zinazoendelea katika kata hizo.

Aliesema mji wa Arusha ni miongoni mwa miji muhimu katika maendeleo ya Tanzania kutokana na umaarufu wake na kuwa mji wa kitalii na biashara.

Kwa mujibu wa katibu huyo, mji huo umeiletea sifa kubwa Tanzania na kuufanya makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kituo muhimu cha mikutano ya kimataifa.

Ameongeza kuwa amani ikitoweka katika eneo hilo, sifa zake zote zitapotea na kukosa mvuto wake wa kitalii, kibiashara na shughuli za kimataifa.

Maalimu Seif, ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, amesema wakazi wa Arusha wana kila sababu ya kujivunia maendeleo na rasilimali zilizopo, yakiwemo madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana Arusha peke yake duniani kote.

Akizungumzia kuhusu kampeni, Maalim Seif amevitaka vyama vya  siasa kufanya kampeni za kistaarabu na kuvumiliana ili kutunza na kulinda amani iliyopo ambayo ni rasilimali kubwa kwa maendeleo ya nchi.

Alisema vyama vingi havikuja kwa lengo la kuwagawa au kuwafitinisha Watanzania, bali kutoa fursa kwa wananchi kuchagua chama au kiongozi wanayemtaka kwa uhuru.

Pia amewaomba viongozi wa vyama vya siasa kushindana kwa hoja na kuachana na tabia ya kuwalazimisha na kuwanyanyasa wananchi na kupelekea kuwakosesha haki na uhuru wao wa kuchagua na kuchaguliwa.

Wagombea udiwani kwa kata za Themi na Kaloleni kupitia CUF Lobora Petro Ndarpoi na Darwesh Abbass Ramadhan, kwa upande wao wamewaahidi wakaazi wa maeneo hao kuwatatulia kero zinazowakabili kwa muda mrefu ukiwemo upungufu wa ajira kwa vijana pamoja kuimarisha huduma za elimu mashuleni.

Wamesema maeneo hayo yana utajiri mkubwa wa viwanda lakini vingi kati ya hivyo havifanyi kazi vizuri, na hivyo kupoteza fursa za ajira kwa vijana, na kwamba iwapo watachaguliwa watashirikiana na halmashauri kuvifufua na kuviendeleza kwa maslahi ya wananchi wa Arusha.

Uchaguzi mdogo wa madiwani kwa kata 26 nchini, unatarajiwa kufanyika Juni 16 mwaka huu baada ya madiwani waliochaguliwa katika kata hizo kupoteza sifa na wengine kufariki.

na Hassan Hamad, Arusha, Tanzania Daima

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO