Kata ya Kaloleni
Mbunge wa Arusha Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, Mh Godbless Lema akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za chama hicho kuwania Udiwani wa Kata ya Kaloleni, mkutano uliofanyika eneo la Ekenya (mashariki ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid) siku ya Mei 30, 2013. Katika Mkutano huo Lema aliainisha ufisadi mkubwa wa jumla ya sh 12 bilioni uliofanywa na watumishi wa Halamshauri ya Manispaa ya Arusha akirejea taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka unaoishia 2012, ikiwemo kutowasilishwa kwa makusanyo ya ushuru mbalimbali na matumizi mengine kukosa nyaraka za kuthibitisha matumizi yake.
Umati wa wananchi na baadhi ya viongozi katika mkutano huo
Themi Relini
Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha Mjini, Martin Sarungi (kulia) akiwa na Mgombea wa Chadema Kata ya Themi, “Kabouru” (katikati) katika mkutano wa Kampeni eneo la Relini uliofanyika Mei 31, 2013
Diwani wa Chadema Halmashauri ya Moshi, Mh Hawa Ali akiwa jukwani kuhutubia wananchi waliojitokeza katika mkutano huo
Kiongozi wa Vijana wa Chadema Korogwe na Mjumbe wa Baraza la Kanda ya Kaskazini Chadema, Bi Aminata nae alipata wasaa wa kuzungumza mkutanoni hapo
Huyu ni Anrose, mwana mama ambaye ana nia ya kuwania Ubunge mwaka 2015 katika Jimbo analoongoza Mh Lyatonga Mrema (TLP) kwa sasa.
Kiongozi wa Vijana Chadema Wilaya ya Hai, Mss Doris Cornel akifafanua jambo mkutanoni hapo
Diwani wa Kata ya daraja Mbili, Mh Msofe nae alikuwepo mkutanoni hapo kumnadi mgombea wa Chadema
Mjumbe wa Halmashauri ya Mji Mdogo wa Usa River, Arumeru Mashariki Mh Josephine Annaely akisisitizia umuhimu wa wananchi kutumia fursa ya kupiga kura waliyoipata kwa manufaa yao kwa kuchagua viongozi wanaofaa
Mwenyekiti wa Vijana wa CHADEMA WIlaya ya Arusha Mjini, Noel Olevaroya akihutubia. Nole alitumia nafasi hiyo kukemea vikali matendo ya baadhi ya wanasiasa wanaohubiri udini na ukabili kwa nia ya kuwagawa watanzania ili wawatawale ama wapate manufaa yao kisiasa, na kudai kwamba hali hiyo ikiachwa iendelee italeta kadhia ambayo hakuna mtu atakayekuwa salama na watanzania hawataulizia tena dhahabu na mali zao viko wapi.
Mgombe mwenyewe wa Udiwani Kata ya Thei kupitia Chadema kimwaga sera zake
Bossi mzito wa Arusha255 akibadilishana mawazo na waheshimiwa madiwani na vicheko vya hapa na pale mkutanoni hapo
Kata ya Kimandolu
Mpiga Kampeni mkuu wa mgombea wa Chadema Kata ya Kimandolu Bw Derick Magoma akimnadi mgombea wake Mch Rayson Ngowi katika mkutano uliofanyika jana jirani na City Link Hotel, Kimandolu.
Mgombea wa Chadema Kata ya Kimandolu Mch Rayson Elishadai Ngowi akijinadi kwa wapiga kura katika mkutano wa kampeni zake uliofanyika eneo Pride Msikitini-Kimandolu tarehe 30 Mei, 2013
Meneja Kampeni wa mgombea wa Chadema Kata ya Kimandolu..Bw Magoma Derick Magoma (mwenye suti) akitafakari jambo katika jukwaa la viongozi wakuu
Mgombea wa Chadema Kata ya Kimandolu Mch Rayson Nowi akisalimina na mdau wake huku bosi wa Arush255 akishuhudia
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Pride, Kimandolu. Picha zote na SeriaJr
0 maoni:
Post a Comment