Mbunge wa Rombo (CHADEMA) Mh Joseph Selasini akitoa ufafanuzi wa taarifa kuhusu wabunge wenzake waliokuwa wameshikiliwa na Polisi jana kuachiwa kwa dhamana ya Polisi asubuhi ya leo bila kufikishwa Mahakamani kama ambavyo walitarajia.Selasini alikuwa akizungumza na watu waliokuwa wamejiandaa kuwadhamini wenzao takribani 70 waliokamatwa jana sambamba na wabunge, Tundu Lissu, Joyce Mukya, Mustafa Akoonay na Mzee Said Arfi.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo anaesimimia Kurugenzi ya upashanaji habari na sera wa Chadema, Mh John Mnyika akitoa taarifa na msimamo wa chama juu ya maziko ya kiongozi wao aliyekufa kwenye bomu Jumamosi na alichodai kuwa ni njama za CCM kutaka kuharibu ushahidi ama kuwatorosha mashahidi walioshuhudia wanaodaiwa kuwa askari ambao waliwapiga kwa risasi na baadhi wakidai walimuona mipuaji bomu na sare za jeshi hilo.
Mnyika amesema kwasababu Jeshi la Polisi limedhamiria kuhakikisha marehemu huyo hataagwa kwenye eneo lolote la wazi kwa mikutano Jijini hapa, basi Chadema wameamua kwa maafikiano na familia ya wafiwa kwamba marehemu ataagwa Kanisani na mazishi yake yatafanyika hapa Arusha eneo ambalo litatajwa baadae.
Mwanasheria Mabere Marando akifafanua jambo kwa Mh John Mnyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo. Wanaoshukudia ni Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Mh mani Golugwa (katikati) pamoja na afisa wa chama makao makuu.
Wabunge wa Chadema, Grace Kiwhelu (katikati) na Vicent Kiboko Nyerere (kushoto) wakiwasili katika viwanja vya Mahakama
Mbunge wa Kawe, Mh Halima Mdee akiwasili Mahakamani hapo
Jihn Mnyika akibadilishana mawazo na watu wa Arusha katika viwanja vya Mahakama hii leo
Wabunge wakipiga stori. wanaotazama mbele, kutoka kushoto Vicent Nyerere, Joseph Selasini, Mh Akoonay na Ezekia Wenje
Mbunge wa Rombo akiongea na waandishi wa habari na kutoa masikitiko yake kwa kitendo alichodai kushuhudia kwa mara ya kwanza kwa askari Polisi kuyapia na kuhabiru magari na pikipiki za raia.
Wabunge wa Chadema wakiongozwa na Mh Selasini wakiwa na furaha
Mh Selasini, Mh Wenje, Mh Nanyaro na waau wengine wakifurahia jambo mahakamani hapo
Wakili Marando, Katibu wa Kanda ya Kaskazini Chadema Amani Golugwa na maofisa wa Chadema makao makuu wakiwasili viwanja vya Mahakama
Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mwenyekiti BAVICHA, Jihn Heche, Mwenykiti Vijana Arumeru Mashariki Methew Kishili na Bossi Mzito wa Arusha255 wakipiga stori mbili tatu katika viwanja hivyo
Kijana huyu alikuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea wasiwasi wa maisha ya pacha mwenzake ambaye amelazwa hospitali ya Seliani kufuatia kuumia katika mlipuko wa bomu jumamosi na sasa anafuatiliwa na maaskari kanzu hospitalini wanaodaiwa kuvaa majoho ya madaktari kwa nia ya kutaka kumtorosha ndugu yake ambaye ameelezwa kushuhudia kila kitu wakati bomu likirushwa hadi anapigwa risasi na mtu aliyevalia nguo za kiaskari.
0 maoni:
Post a Comment