Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN NA UJUMBE WAKE NCHINI CHINA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Madaktari wakati alipotembelea Hospitali Kuu ya Mjini Nanjing jimbo la Jiangsu Nchini China akiwa katika ziara ya kiserikali katika kukuza uhusiano.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, (wa tatu kulia) na ujumbe wake alipozungumza na Uongozi wa Hospitali ya Mji wa Nanjing katika jimbo la Jiangsu, wakati alipotembelea Hospitali hiyo akiwa katika ziara ya kiserikali katika kukuza uhusiano na mashiririkiano ya kiuchumi .

Baadhi ya madaktari wa Drum Tower Hospital wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa na ujumbe wake akizungumza katika kikao cha kubadilishana mawazo na uongozi wa Hospitali hiyo akiwa katika ziara ya mualiko wa Serikali ya jamhuri ya Watu wa China .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto)Mama mwanamwema Shein kulia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha,Uchumi na Mipango ya maendeleo Omar Yussuf Mzee,wakianagalia picha baada ya kumalizika kikao cha pamoja na uongozi wa Drum Tower Hospital.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) pamoja na ujumbe aliofuatana nao wakiangali Picha Mfano wa majengo ya Drum Tower Hospital ,walipokuwa wakitembelea sehemu mbali mbali za ofisi ya Hospitali hiyo,katika ziara ya Kiserikali nchini China,kwa mualiko wa Serikali ya jamhuri ya Watu wa Nchi hiyo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) pamoja na ujumbe aliofuatana nao wakitembelea sehemu mbali mbali za Drum Tower Hospital iliyopo katika Mji wa Nanjing Jimbo la Jiangsu chini China,kwa ziara ya Kiserilkali,kwa mualiko wa Seikalia ya jamhuri ya Watu wa Nchi hiyo,(kulia) Rais akiwa Prof Dr.Yi Tao Ding, wa Chuo Kikuu cha Afya katika DrumTower Hospital.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiapata maelezo kutoka kwa Prof Zhou Chang,wakati alipotembelea sehemu za Uchunguzi wa Afya ya binadamu kwa kutumia kompyuta maalum katika Drum Tower Hospital,Mjini Nanjing katika jimbo la jiangsu kwa ziara ya kiserikali.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wake,pia na Uongozi wa Drum Tower Hospital,baada ya kumaliza kutembelea Ofisi pamoja na Sehemu mbali mbali za kutoa huduma ya Afya,akiwa katika ziara ya mualiko wa Kiserikali nchini China.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Gavana wa Jimbo la Jiangsu jana alipofika katika Mkahawa wa Chunzaige Mjini Nanjing,akiwa katika ziara ya mualiko wa Kiserikali wa jamhuri ya Watu wa China.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, na ujumbe wake wakiwa katika mkutano wa pamoja na Gavana wa Jimbo la Jiangsu jana alipofika katika Mkahawa wa Chunzaige Mjini Nanjing,akiwa katika ziara ya mualiko wa Kiserikali wa jamhuri ya Watu wa China,[Picha na Ramadhan Othman,China.]

 

 

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO