Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MGOMBEA UDIWANI WA CUF AMWAGA CHOZI JUKWAANI ARUSHA;

Mgombea udiwani Kata ya Elerai kwa tiketi ya CUF, John Bayo akitambulishwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maali Seif Sharif Hammad katika mkutano wa kampeni wa chama hicho Elerai


Uchaguzi wa udiwani kwenye jimbo la Arusha umechukuwa sura mpya baada ya mgombea wa udiwani wa chama cha wananchi (CUF)kwenye kata ya Elerai John Gilbert Bayo kuangua kilio jukwaani wakati akinadi sera zake mbele ya wananchi, wakazi wa kata hiyo na katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.

Mgombea huyo aliangua kilio hicho baada ya kuwaambia na kuapa mbele ya wakazi hao wa kata yake kuwa hakuwahi kupokea fedha kiasi cha 50 milion kwa ajili ya kupata muafaka wa meye wa jiji la Arusha kama chama cha demokrasia na maendeleo wanavyodai na kuwa hata weza kukiuka maadili na kuwatosa waliomchagua.

Akizungumza kwenye kampeni hizo katibu mkuu wa CUF na makam wa kwanza wa serekali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar Seif Sharif Hamad aliwataka wakazi wa kata ya Elerai kuwachagua wagombea wa chama hicho kwani chama hicho kimekuwa kikihimiza umoja na Amani wakti wote.

Maalimu Seifu akabainisha kuwa Mgombea wa CUF kwenye kata ya Elerai John Bayo ni mtu makini na mchapakazi na kuwa wao hawapo kumfukuza mtu bali wananchi ndio watakao amua hatma ya viongozi wanaowataka kwani sisi CUF ndio walimu wa amani hapa nchini kama tungekuwa hatuhubiri amani Zanzibar isinge kalika baada ya uchaguzi mkuu kwani chaguzi zote tuliweza kushinda lakini tulipokwa ushindi.

“Sisi CUF ndio wahubiri wa amani kwani tangu mwaka 1995 tumeshinda chaguzi zote lakini kwa hekima na busara tuliwakataza vijana kuingia barabarani kudai haki yao lakini leo matunda ya busara si mnayaona”alisema Maalimu Seifu.

Zanzibar wananchi waliishi kwa uhasama na tukaona kama tutaenda hivyo kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 basi kutaweza kutokea mchafuko hivyo mimi na Rais mstaafu Karume tulikaa na baaadae vyama na hatimaye wananchi zaidi ya 66%akaidhinisha muafaka huu ni uamuzi wa busara na leo ndiyo iliyozaa serekali ya umoja wa kitaifa.

Maalimu akatanabaisha kuwa CUF inaimani na John Bayo kwa kuwa ndiyo chaguo la wananchi wa kata hiyo na kuwataka kumpa kura zote iliawe diwani wao na kusema hivi sasa Zanzibar imetulia baada ya mwafaka ule na haya ni matunda ya chama hicho na kuwa hawatajuta kuchagua mgombea wa chama hicho kwenye kata zote waliosuimamisha wagombea.

Naye mgombea wa udiwani wa Kata ya Elerai John Bayo alisema kuwa akichaguliwa atapambana na kero mbalimbali zinazowakabili wakazi wa kata hiyo ikiwemo kutoa michango ya kununua madawati na majembe kila mwaka kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Bayo akawataka wakazi wa kata hiyo kuwaonyesha kuwa hakuchaguliwa na mafuriko ya chadema kwa kumpigia kura ya ndiyo kwenye uchaguzi huo siku ya tarehe 16 mwezi huu na kuwa majengo ya Zahanati wao hawataki zahanati bali kituo cha Afya hivyo wakimpa ridhaa hizo zitakuwa kipaumbele chake.



SEIF AWATAKA WAKAZI WAKATA YA ELERAI KUHUBIRI AMANI NA KUWAKATA WOTE WASIOTAKA MANI

Maalim Seif ThemiWakazi wa kata ya Elerai wametakiwa kuhubiri amani na mshikamano na kukataa wale wote ambao hawaitakii amani Mkoa wa Arusha kwani wamekuwa wakiwaumiza kiuchumi na kimaendeleo na kuwa vurugu na maandamano kwao hayana tija badala yake ni hasara kwa uchumi na maendeleo ya mkoa wao.


Kauli hiyo imetolewa na makamu wa kwanza wa serekali ya umoja wa kitaifa(SMZ)Maalim Seif Sharif Hamad wakati akiongea na wakazi wa kata hiyo alipokuwa mgeni rasmi kwenye kampeni za uchaguzi wa kata hiyo.


Sharif hamad aliwataka watanzania kutobaguana kwa visingizio vya ukabila udini na aina yeyote ya ubaguzi kwa minajili ya kuvurga amani na mshikamano wa taifa letu na kuwa siasa ni maisha ya watanzania wote hivyo kila mmoja wetu anawajibu wa kutunza amani na mshikamano sanjari na kuacha ushabiki kwenye siasa.


“Ndugu zangu wana Arusha siasa ndiyo maisha yetu na vijana ndio msingi wa taifa kwani ndiyo nguvu kazi sasa hawa wakitumika vibaya kwa maslahi ya wachache kufanya vurugu na maandamano tutakuwa tunaelekea wapi”alihoji Maalim Seif.


Makamu huyo alisema watanzania wote bila kujali rangi,ukabila,na udini wanahaki sawa za kupata mgawanyo wa kiuchumi hapa hakuna ambaye hana hati miliki na nchi hii kwani nchi hii ni yetu sote bila kujali itikadi za vyama.


Alisema anashangaa kuona nchi hii yenye rasilimali lukuki na ardhi isiyokataa mazao yeyote hapa dunia ikiwa katika hali mbaya ya kukosa chakula wakati imejaaliwa neema kubwa hii ndiyo sera za chama cha mapinduzi kilipotufikisha na kuwataka watanzania kuacha ushabiki wa kisiasa na kujiuliza tumekosea wapi ilituweze kuyapatia majibu sahihi jmatatizo yetu.

STORI NA PICHA: WOINDE SHIZZA (LIBENEKE LA KASKAZINI)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO