Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: SHOW YA LADY JAYDEE NYUMBANI LOUNGE JUNI 14, 2013 ……ANGALIA JINSI ILIVYOFANA

 

 

Mwanadada Judith Mbibo aka Lady Jaydee usiku wa kuamkia Jumamosi ya June 15 amefanikiwa kuweka historia kwenye muziki wa Tanzania kwa kulijaza eneo zima la Nyumbani Lounge alipokuwa akifanya show yake ya kuadhimisha miaka 13 tangu aanze muziki. 

DSC_4275

Katika show hiyo, Lady Jaydee amesindikizwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Juma Nature, Sugu, Profesa Jay, Wakazi, Grace Matata na wengine. Pia Jaydee ameitumia siku hiyo kuzindua albam yake mpya, Nothing But The Truth na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Hizi ni picha za show hiyo.

DSC_4279

DSC_4285

DSC_4288

 

DSC_4293

DSC_4299

DSC_4300

 

DSC_4445

DSC_4447

DSC_4449

DSC_4466

DSC_4261

 

PICHA ZOTE NA Bongo5.Com


PICHA ZINGINE ZA SHOW YA LADY JD, AOGA FEDHA, SUGUU NA PROFESA JAY WANG'AA JUKWAANI KWA MUJIBU WA BIN ZUBEIRY BLOG

Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JUNI 15, 2013 SAA 11:00 ASUBUHI ONYESHO la mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ kutimiza miaka 13 katika muziki, limefana usiku wa kuamkia leo katika eneo la maegesho ya magari kwenye ukumbi wa Nyumbani, Lounge, eneo la Kinondoni, Dar es Salaam kwa mamia kujitokeza kiasi cha kujaza eneo hilo, hadi kupishana ikawa taabu. Watoto wa mjini wanasema ilikuwa funika bovu- ndiyo shoo hiyo ilikuwa nzuri mno, ya kistaarabu, yenye mashamsham ya aina yake.

Jide akikumbatiana na Profesa Jay

Jay akipagawisha

Jay akisema na nyomi

Mzee Kitime akimpiga picha Komando Kalala wakati anaimba 

Komando Kalala na mkewe jukwaani

Msanii Mango Star na nyoka

Mango Star na nyoka

Wasanii nguli wa Hip hop waliomsindikiza Jadyee katika shoo hiyo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Joseph Haule na Juma Nature na kundi lake wanaume Halisi nao walifanya mambo mazuri jukwaani kiasi cha kuiongezea utamu shoo hiyo. Kufika saa 3:00 usiku tayari Machozi Band inayomilikiwa na Jide ilikuwa jukwaani kuanza kutumbuiza kabla ya kumpisha rapa Wakazi kutoka Ukonga, baadaye bendi ya M ikiongozwa na Grace Matata kwa shoo za utangulizi. Saa 5:00 usiku, Jide akapanda jukwaani na kuibua shangwe nzito kutoka kwa mamia waliokuwa wamefurika katika eneo hilo. Jaydee alianza na wimbo wa Nilishakuwaga na Wangu, baadaye akaimba Nakuhitaji, Moto, Mambo Bado, Yeye, Malaika, Siri Yangu, Wanock Nok kisha kumalizia na Single Boy katika awamu ya kwanza. Baada ya hapo, Jide akasema ilipotimu Saa 6:00 usiku ameingia katika mwaka mpya tangu azaliwe hivyo mashabiki wakamuimbia ‘Happy Birth Day’ kisha akateremka kwenda kukumbatiana na mama yake mzazi, Martha Mbibo na kumpa zawadi ya fedha zote alizokuwa ametuzwa jukwaani. Jide alirejea jukwaani na kuimba kwa ufupi nyimbo alizowahi kurekodi na wasanii Man Ngwair na Langa Kileo ambao hivi sasa ni marehemu, kabla ya kumpisha Mh. Mbunge wa Mbeya Mjini, Sugu ambaye aliimba nyimbo tatu tu, lakini alisisimua mashabiki ile mbaya. Sugu alianza na Hakuna Matata akimshirikisha Mkoloni, Sugu na kumalizia na Mambo ya Fedha ambao ulimrejesha jukwaani Jide. Kutoka hapo, ikawadia zamu ya Wanaume Halisi kutoka Temeke, wakiongoza na Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’, ambao nao walifanya balaa vile vile na kuurusha umati ile mbaya.

Msanii M2 The P akizungumza jukwaani

KR Mulla

Sir Nature

Nature na Doro

Sinta akimpiga picha Nature

Wakati Nature anaimba, mpenzi wake wa zamani Christine Manongi ‘Sinta’ alikuwa bize kumpiga picha ‘mzee’ wake wa kitambo, kiasi cha mmoja wa viongozi wa kundi hilo, Kiboya kupora kipaza sauti na kutamka Baba Sinta akimtania Nature, jambo ambalo liliwafanya watu washangilie.    Nature kabla ya kuanza kuimba alimpandisha jukwaani msanii M 2 P aliyezushiwa kifo wakati akiwa amelazwa Afrika Kusini sambamba na Man Ngwair. MP alisalimia na kushukuru kwa dua za Watanzania wakati akiwa taabani wadini, kwani zimemponya na akatumia fursa hiyo kumuombea swahiba wake Ngwair apumzishwe kwa amani peponi. Ndipo Wanaume wakaanza vitu vyao, wakipiga nyimbo za Sonia, Hakuna Kulala, Mzee wa Busara, Ladhia, Haipotei, Dance With Me na Jimwage. 

Jaydee na mama yake

Jaydee akikusanya fedha alizotuzwa

Anaziweka kwenye boksi kabla ya kweneda kumpa mama yake. Alyeshika boksi ni King Kiboya

TK wa M Band...

Maeneo kama haya Mh Sugu huwa si mkali...anajua kutabasamu

Rapa kutoka Ukonga

Alikuwepo...Mgaya Kingoba Mhariri wa Michezo gazeti la Habari Leo

Kutoka kulia Baraka Msilwa, Francis Kifukwe na mkewe

Wanaume walipoondoka akaibuka msanii mcheza ngoma za asili huku akichezea nyoka, Mango Star ambaye aliwaacha watu midomo wazi pale alipokuwa akimnyonya nyoka upande wa kichwani. Akafuatia mkongwe Komando Hamza Kelele ambaye kwanza alimpandisha mkewe, Stella John Momose Cheyo jukwaani kumtambulisha, kisha akaimba nyimbo na Tumetulia. Ikawadia zamu ya Profesa Jay, ambaye aliimba Joto Hasira pamoja la Lady Jaydee, baadaye, Teja, Yahya na Joto tena. Jaydee akateremka na kumuacha Jay amalizie shoo naye akamalizia vizuri kwa nyimbo za Hapo Vipi, Nikusaidiaje na Kamili Gado. Watu kadhaa waliofika Nyumbani Lounge kushuhudia shoo hiyo walilazimia kugeuka na kuondoka kwa sababu ukumbi ulikuwa ‘umejaa na hakuna pa kukanyaga’. Kwa ujumla shoo hiyo ilipendeza, ilikuwa bab kubwa.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO