Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: ZIARA YA RAIS KIKWETE SUNDERLAND AFC

 

Imeandikwa kwa ushirikiano wa Urban Pulse na Freddy Macha

Ramani ya chuo kitakachojengwa Dar es Salaam

  Rais akionyeshwa ramani ya mpango wa chuo cha mpira kitakachojengwa Dar es Salaam. Sisi (kama hawa wenzetu) tunao wachezaji wenye vipaji. Tunao pia uchungu kwa nchi yetu; na kama alivyosema Rais Jakaya Kikwete alipoitembelea klabu ya Sunderland AFC Jumapili 16 , Juni, “Watanzania tunapenda michezo.”


Mara ya mwisho Tanzania kusikika kimataifa michezoni ilikuwa 1980 wakimbiaji Filbert Bayi na Suleiman Nyambui walipotwaa medali za Olimpiki, Moscow na timu yetu ya taifa ya mpira iliposhiriki fainali za kombe la Afrika mjini Lagos , Nigeria...

kids playing football at Academy of Light-oic by Urban PulseWatoto wadogo wakisakata gozi Academy of Light. Samaki mkunje angali mbichi... Kiu ya miaka 30 imezungumziwa na kujadiliwa sana hatimaye tumeanza kuzoea kushangilia wengine. Tumezoea mtazamo huu kiasi ambacho ni rahisi kwa shabiki wa Kitanzania kuijua timu nzima ya wachezaji wa Manchester United au Barcelona kuliko Yanga na Simba. Kati ya sababu kuu za kushindwa huku kila mwaka ni kutowekezea katika matayarisho na kutochangamkia tulicho nacho. Wenzetu wa Hispania, Brazil, Uingereza, Nigeria, Ivory Coast, Kenya nk wanatuzidi moja. Wanajipenda. 


Mheshimiwa Rais mwenyewe, aliwaeleza wanahabari waliomhoji kwamba zamani alikuwa mchezaji wa mpira wa kikapu. Ni vizuri kuwa na kiongozi mpenda michezo. Na mwaliko Rais aliopewa na mwenyekiti wa klabu ya Sunderland AFC , Ellis Short umeotesha si tu mbegu ; sharti tuanze kuchangamkia tulicho nacho. Mpenda kwao hutunzwa. Jamani, eh, tuichangamkie dili. Dili yenyewe ni ipi?Ramani ya Mpango wa chuo kitakachojengwa Dar es Salaam

  Rais Kikwete akitembezwa viwanja vya Academy of Light. Mkono wake wa kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara klabu ya Sunderland AFC, Gary Hutchinson na kulia kwake, Profesa Anna Tubaijuka, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Rais na msafara wake uliomhusisha pia Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara, walielezwa kuwa kampuni ya kimataifa ya umeme –Symbion Power- itaanza mara moja kujenga chuo (Sports Academy) cha kufundishia mpira jijini Dar es Salaam. Afisa Mkuu wa Symbion, Bw. Paul Hinks alisema punde ujenzi utakapomalizika, Sunderland AFC itaanza utaalamu na uzoefu wake kwa kutoa mafunzo ya mchezo huu unaopendwa Tanzania. Kazi hii ina hatua mbili. Ya kwanza Dar es Salaam, ya pili, kujenga na kuendeleza mpira Tanzania ili kuufikisha hatua ya juu, aliahidi Hinks.

Rais Kikwete akionyeshwa kijana aliyeumia anauguzwa hapo hapo chuoni

Rais na wageni wakielezwa namna vijana wachezaji wanavyohudumiwa wakiumia. Majeruhi ni Tom Beedling na mganga wake(Physiotherapist), Jamie Oldroyd. Mheshimiwa na msafara ulionyeshwa zana mbalimbali zilizomo chuo cha Academy of Light yakiwemo mabwawa ya kuogelea, sehemu za matibabu, mazoezi ya viungo, vyuma na mashine (Gym), viwanja vya ndani na nje, nk. Huo ndiyo mpango wenyewe.Rais Kikwete akiongea a watoto

  Mkuu wa nchi akiongea na watoto wanaosomea Academy of Light. Kila jambo linalohusisha fani hii hufunzwa hapa: sayansi, kompyuta, viungo, afya, nk. Tumeshaletewa vifaa vya mapishi; sasa “kazi kwetu. “ Siri kuu ya klabu na nchi zinazotuzidi duniani kimichezo ni matayarisho ya aina hii. Klabu maarufu ya Barcelona (na Spain yenyewe ambayo ni viongozi wa kandanda ulimwenguni sasa hivi) ni kuwa na wachezaji waliojengwa vizuri wakiwa watoto. Lionel Messi, Xavi Hernandez, Andreas Iniesta walianzia chuo cha La Masia chenye zaidi ya wanafunzi 300. La Masia ilianzishwa mwaka 2002 na matokeo yake ndiyo haya.Rais Kikwete akiongea na Wanahabari wa SKY

  Rais akiongea na wanahabari wa SKY baada ya matembezi uwanja wa Stadium of Light na chuo cha Academy of Light kwa muda wa saa nne. Mfano mwingine mzuri zaidi (na unaotufaa sisi Tanzania) ni ule wa klabu ndogo isiyojulikana sana Bongo yaani Southampton FC, kusini ya Uingereza. Southampton Football Club ina chuo ambacho miaka ya karibuni kimechanusha wachezaji wazuri sana na watatu wameshajulikana ligi ya Uingereza : Theo Walcott (Arsenal), Gareth Bale (Tottenham) na Alex Oxlade- Chamberlain (Arsenal). Gareth Bale ni mmoja wa washambuliaji hatari duniani na klabu kubwa kubwa ikiwepo Real Madrid zinamwinda kama swala. Na ndiyo maana Rais Kikwete alipoulizwa kwanini katembelea Sunderland (iliyoshika nafasi ya 17 ndani ya timu 20 zilizoshiriki ligi ya 2013) na sio Chelsea, Liverpool au Manchester City akajibu wao ndiyo walio tayari kutusaidia. Ikumbukwe kwamba Academy of Light, ni kati ya vyuo vinavyoheshimika Uingereza nzima. Naam. Wako tayari kutusaidia. Tuangalie tatizo letu kuu.

Kiwete akiwa na watoto Sunderland© 2013  Frank Eyembe

  Rais Kikwete akiwa na watoto wa kike na kiume wanaojifunza mpira viwanja vya Academy of Light. Hatuamini sana faida ya michezo. Hatuwezi kukataa si wazazi wengi wa Bongo wanaoamini kwamba mtoto wao akizama michezoni atajenga ajira. Hatuchangamkii michezo kiajira kama walivyo wenzetu. Mwangalie mchezaji mashuhuri Wayne Rooney wa Manchester United ambaye ingawa hakusoma sana leo katajirika, anasaidia familia na jamii yake. Mifano ni mingi sana. Afrika tunae mchezaji mstaafu wa Nigeria, Nwankwo Kanu (kaacha kucheza akiwa na umri mbichi wa miaka 36 na sasa tajiri); licha ya kuwa mgonjwa wa moyo akiwa mtoto, ilibidi atibiwe kutokana na kipaji chake na hatimaye akaiongoza Nigeria kushinda kombe la Vijana Afrika (1993), Olimpiki (1996) na tuzo kadhaa akiichezea kazuzu, Arsenal (1999-2005). Leo anafanya mengi Nigeria ikiwepo kudhamini hospitali ya watoto wagonjwa wa moyo. Tubadili utayarishaji wetu. Twahitaji mosi, kuchangamkia michezo, pili, kuwasaidia watoto na vijana wetu wanaoanza ngazi za chini, vijijini hadi pembe za chaki mijini. Uwanja wa Stadium of Light

Leo kwetu Tanzania wachezaji wazuri “huanza” kuingizwa ulingoni wakiwa na umri wa miaka 17 kuendelea. Wenzetu wanaoshinda huzingatia methali ya “samaki mkunje angali mbichi.” Watoto wanaoonekana kuwa na vipaji kimichezo huanza kuokwa na kupewa misaada ya hali na mali, wakiwa na umri mdogo wa miaka mitano. Rais alijionea mwenyewe watoto hawa na kufurahia na wenzake akiwemo, Mheshimiwa Peter Kallaghe ambaye pamoja na Ubalozi wa Tanzania , London waliiratibu ziara na shughuli hii muhimu kitaifa.Rais akiwa na Watanzania wakazi New Castle na Sunderland-pic by Urban Pulse

  Rais na viongozi wenzake wakiwa na Watanzania wakazi wa New Castle na Sunderland waliofika kumsalimu. Waliokaa pamoja na wananchi ni toka kushoto, Balozi Peter Kallaghe, Bw Ellis Short (Mwenyekiti wa Sunderland AFC), Rais Kikwete, Dk Fenella Mukangara (Waziri mhusika Michezo) na Bw Paul Hinks wa Symbion Power itakayojenga chuo Tanzania.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO