Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Breaking News: Mh Mbowe, Lema Wanusururika Kulipuliwa na Bomu Mkutano wa Chadema Kufunga Kamapeni za Udiwani Viwanja Vya Soweto Jijini Arusha; 3 Wafariki, Wengi Wajeruhiwa

Uwanja wa Soweto ambapo Mkutano wa Chadema kufunga kampeni za kuwania Udiwani Kata ya Kaloleni Jijini Arusha ulikuwa unafanyika umegeuka kuwa uwanja wa vilio baada ya kinachodhaniwa kuwa bomu kulipuka na kuua watu watatu na zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya huku baadhi yao wakiwa wamevunjika miguu.

Katika Mkutano huo walikuwapo pia Mwenyekiti wa Chadema naa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema sambamba na viongozi wengine wa Chadema Mkoa wa Arusha lakini bahati nzuri Mbowe na Lema ambao walokuwa vinara katika Mkutano huo hawakudhurika moja kwa moja na mlipuko huo.

Mlipuko huo ulitokea mbele ya gari ambalo lilikuwa ni jukwaa la matangazo mara baada tu ya Mh Mbowe, Lema na viongozi wote waliokuwa jukwaa kuu kushuka chini na kujichanganya katikati ya watu wakikusanya michango ya watu, hali inayoashiria mrushaji huenda lilenga kuwajeruhi viongozi hao.

Lakini jambo la kushnagaza kidogo ni milio ya risasi za mto iliyofuatia mfululizo baada tu ya kishindo cha mlipuko wa bomu na hata baadhi ya majeruhi wameelezwa kukutwa na risasi mwilini na pia inadaiwa maganda kadhaa ya risasi yameokotwa viwanjani hapo. Blogu hii ilishuhudia mama mmoja akiwa na tundu kubwa kifuani linalodhaniwa kutokana na risasi ya mto. Haijaweza kufahamika waliofyatua risasi hizo ingawa askari Polisi walikuwepo wengi na wengine wakivalia kiraia.

Miili ya marehemu na majeruhi walipelekwa hospitali ya Mt Meru lakini hawakupokelewa kwanza baada ya kilichoelezwa ni vurumai iliiyoletwa na mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa na hasira baada ya wenzao kuuwawa, na hivyo baadhi kuhamishiwa hopsitali nyingine kama Seliana na AICC kwa matibabu ya haraka.

Baadhi ya majeruhi ni viongozi wa Chadema ngazi ya Kata, Wilaya na Mkoa wa Arusha, sambamba na wananchi wa kawaida wakiwemo watoto waliofika mkutanoni hapo.

Mkutano wa leo ulivunja rekodi ya mahudhurio viwanjani hapo.. lakini ulikuja kuharibika baada ya kutokea mlipuko huo haotuba zikiwa zimeishamalizika na baadhi ya watu wakiwa wanatawanyika kuelekea majumbani huku zoezi la kuchangisha pesa likiendelea, kitendo kilichowazuia hata wakusanyaji michango kushindwa kumalizia zoezi hilo…

Hali ikiwa bado tete viwanjani hapo, magari kadhaa ya askari polisi yalifika huku askari wakiwa na silaha lakini walilazimika kupiga mabomu ya machozi kadhaa hewani na kisha kuondoka kutokana na baadhi ya wananchi waliokuwa na hasira kuwafuata na kupaza sauti wakitaka wawaue pia.

Kijana mmoja muuza machungwa aliieleza blogu hii kuwa aliyerusha bomu hilo alitokea upande wa nyuma ya jukwaa kuu na badae kukimbilia nyumba zilizojirani.

DSC07403

Mbowe - SowetoMwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasili viwanja vya Soweto, Kata ya Kaloleni Jijini Arusha jioni ya leo katika Mkutano wa Chadema kufunga kampeni zake.

DSC07401Mh Mbowe akichangisha pesa mkutanoni hapo sekunde chache kabla ya mlipuko kutokea

DSC07413Hali ilivyokuwa baada ya mlipuko ulioua na kujeruhi vibaya

DSC07407Hali za majeruhi na marehemu wakiwa chini kabla ya kukimbizwa hospitalini

DSC07408

DSC07426Mama huyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja inadaiwa amejeruhiwa na risasi kifuani kama jeraha linavyoonesha, akiwa anahema kwa shida akiwahishwa hopsitalini.

DSC07411

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO