Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

“Zanzibar lazima iwe mamlaka yenye dola”– Maalim Seif

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad amesema muundo wowote utakaokuja wa Muungano lazima Zanzibar iwe na mamlaka kamili ya kidola.

Alisema kinyume na mamlaka kamili rasimu itakayokuja itakataliwa bila ya kigugumizi.

Maalimu Seif Sharif Hamad ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUf) aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Kibandamaiti Zanzibar.

“Wazanzibar wapatao asilimia 66 wametoa maoni yao yenye mamlaka kamili, leo uje na katiba inayokwenda kinyume na matakwa yao, hilo halikubaliki” alisema Maalim Seif.

Akizungumza juu ya mambo ambayo hayapaswi kuwa ya Muungano alisema ni pamoja na uraia, uhamiaji, sarafu, mipaka, polisi na mambo ya nje.

“Tanganyika watoe Pasi za kusafiria zao na Zanzibar zao” alisema Hamad.

Mapema mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu alisema hatarajii kama Tume ya Mabadiliko ya Katiba itapanga maoni ya vongozi wengi wa Juu Tanzania ya kuipa Zanzibar Mamlaka yake.

Chanzo: Mwananchi

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO