Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 24 WA MWAKA WA TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA JIJINI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia washiriki wa kutano, wakati akifungua rasmi Mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza Juni 25, 2013 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Utafiti wa Mitambo ya Nyuklia, Kitengo cha Matengenezo, Yesaya Sungita, wakati Makamu alipotembelea Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha leo, Juni 25, 2013 baada ya kufungua mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza Juni 25, 2013 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa msimamizi wa Mashine ya kutafiti Vyakula na Mazingira, Remigius Kawala, wakati Makamu alipotembelea Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha leo, Juni 25, 2013 baada ya kufungua mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza Juni 25, 2013 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.

Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akionyeshwa baadhi ya maeneo ya Taasisi hiyo, wakati alipotembelea katika Taasisi hiyo iliyopo Njiro jijini Arusha.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo Juni 25, 2013 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia na kusikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Kinga ya Mionzi, Ukaguzi wa  Vifaa, Dkt. Willbrod Muhogola, wakati Makamu alipotembelea Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha Juni 25, 2013 baada ya kufungua mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza Juni 25, 2013 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha, baada ya kuzungumza nao alipotembelea Taasisi hiyo Juni 25, 2013. Picha na OMR

Picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO