Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kili Music Tour 2013 ilivyofana ndani ya jijini Tanga

Msanii wa Muziki wa Hip Hop,Roma Mkatoliki akipanga na kupangua vina vyake wakati wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani,jijini Tanga.

Roma Mkatoliki akiwapagawisha wakazi wa mji wa Tanga waliojitokeza kwa Wingi kwenye Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani,jijini Tanga.

Mkali wa Hip Hop,Prof. Jay a.k.a a.ka The Heavy Weight  MC akikamua vilivyo mbele ya Wakazi lukuki waliofika kwenye viwanja vya Mkwakwani kuona Onyesho la Muziki linaloongozwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Kilimanjaro maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.

Prof. Jay akiendelea kukamua kwenye Onyesho hilo Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani,jijini Tanga.

Prof. Jay akiwashukuru wakazi wa Tanga.

Mwana FA a.k.a Binamu akiimba wimbo wake wa Yalaiti na Mwanadada aliepanda jukwaani kuimba badala ya Msanii alieimba nae wimbo huo.

Binamu akikamua huku shangwe zikitawala.

Msanii wa Muziki wa Taratibu,Maarufu kwa jina la Recho akiimba nyimbo zake mbali mbali wakati wa Onyesho la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani,jijini Tanga.

Mamaa wa Majanga aitwae Snura akiwapagawisha wakazi wa Tanga na goma lake lililoshika hatamu sana hapa nchini (MAJANGA).

Ali Kiba na madansa wake wakitoa Burudani kwenye Onyesho hilo.

Ali Kiba akikamua..........

Mkali wa Hip Hop hapa nchini kwa Mwaka 2012/13,Kala Jeremier akifanya mambo yake mbele ya Mashabiki wake Lukuki waliofika ndani ya Uwanja wa Mkwakwani,Jijini Tanga usiku wa kuamkia leo.

Tanga ilizizima kwa shangwe wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

DJ Mackay akisimamia vyema show hiyo.

Mzee Yusuph akitoa burudani kwa Mashabiki wake wa Jiji la Tanga.

Mambo ya Mwambao....

Meneja wa Bia la Kilimanjaro,George Kavishe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa EATV wanaosimamia zoezi zila la Onyesho hilo.

Wadau Scooby na Baltazary.

Mapacha wa Snura katika Pozz.

Wadau wa EATV.

Toka kulia ni DJ Choka,Kiboya na Dada Ester wakiwakilisha ndani ya Mkwakwani,Tanga.

Wakazi wa Tanga wakikongwa nyoyo zao

PICHA ZOTE NA ISSA MICHUZI

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO