Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

UVCCM MBEYA WATOA UFAFANUZI KUHUSU TUHUMA ZA KAMBI ZA KIJESHI KWA VIJANA MKOANI HUMO

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Mbeya Mjini Malanyingi Matukuta

UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Mbeya Mjini kimesema kuwa Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) wilayani humo kimefikia hatua ya kujichekesha chenyewe kisha kucheka.

Wakizungumza na waandishi wa habari Jijini Mbeya leo, Umoja huo umesema kuwa hatua hiyo ya Chadema inatokana na kuona dalili zote za kushindwa katika uchaguzi mdogo wa kata ya Iyela unaotarajiwa kufanyika June 16,2013.

Katibu wa UVCCM wilayani humo Julius Msaka, amesema kuwa, kutokana na kampeni zinazoendelea katika kata hiyo na baadhi ya wafuasi wa Chadema na viongozi wao kufanya fujo kwa wafuasi wa CCM bila kufanywa lolote, sasa wameamua kujichekesha na kucheka wenyewe.

''Kama vijana, hatutavumilia kuona mwanachama yeyote wa CCM akipigwa na wafuasi wa Chadema kisha akaachwa, tutawalinda wanachama wetu mpaka siku ya uchaguzi na hata kupita'' amesema Msaka.

Amesema kutokana na  viongozi hao kuona dalili za kushindwa, waliamua kutumia Gazeti la Tanzania kuandika habari kuwa CCM inajifua kijeshi kwa maagizo ya Mwigulu nchemba hali ambayo siyo ya kweli.

''Sisi kama vijana wa CCM, tunao utaratibu wa kuwa na makambi kila mwaka mara mbili si kwa ajili ya uchaguzi tu, bali kwa ajili ya kujifunza ujasiliamali, ukakamavu na itikadi za chama chetu na tunawahakikishia kuwa tutaendelea kufanya hivyo bila kuvunja sheria za nchi'' alisema Msaka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo Malanyingi Matukuta, amesema kuwa vijana wa umoja huo ni walinzi wa chama na viongozi wao hivyo kambi waliloweka katika shule ya Sekondari Ivumwe ni la wazi na wala si kwa maagizo ya Mwigulu Nchemba.

''Kwanza tunakanusha habari zilizoandikwa na Tanzania Daima kuwa tumefanya kambi kwa maagizo ya Mwigulu Nchemba na hii ni propaganda ya Chadema ili wapate kura za huruma katika kata ya Iyela'' anasema Matukuta.

Alimshutumu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Mbeya mjini John Mwambigija kuwa alitoa taarifa majukwaani kuwa kuna vijana 600 wa CCM ambao wameweka kampbiu eneo la Itende Sec, Igawilo na Igoma, taarifa alizosema kuwa siyo sahihi.

Alisema eneo walilokuwa wameweka kambi, hata askari Polisi walifika na kupiga picha wakiwa kwenye mchakamchaka na mazoezi mengine lakini ajabu wapinzanzani wao kisiasa hasa Chadema wanadai kuwa wanajifunza mafunzo ya Janjawidi.

''Mafunzo ya Janjawidi ni lazima uwe na mapanga, Bunduki, shoka au visu. Lakini vyote hivyo hatukuwa navyo na wakawakurupusha Polisi wakaja pale lakini hawakukuta madai yao yaliyowaambia kuwa eti tumeteka watu'' anasema Matukuta.

Viongozi hao walitoa wito kwa wananchi wa kata ya Iyela kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kwamba hakuna atakayedhulika na propaganda za wapinzani wao kuwa mgombea Richard Shangwi si mtanzania na siyo Mkristo zimekufa baada ya ukweli kujisimamia na kubainika kuwa ni Mtanzania na ni Mkristo aliyebatizwa kanisa Katoliki mwaka 1963.

Imeandikwa na Gordon Kalulunga, Mbeya (umeipata hapa kwa hisani ya Filbert Rweyemamu)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO