Obama anatarajiwa kwenda Afrika Kusini kisha Tanzania kwa ziara yake ya pili Afrika
Rais wa Marekani Barack Obama ambaye yuko katika ziara yake ya Afrika, amesifu nchi ya Senegal kwa kuwa moja ya nchi zenye demokrasia thabiti barani Afrika.
Akiwahutubia waandishi wa habari nchini Senegal kwa mkondo wake wa kwanza wa ziara yake Afrika,baada ya mazungumzo na rais Macky Sall, Bwana Obama alisema kuwa Senegal iliandaa uchaguzi huru na wa haki pamoja na kuwa na kipindi salama cha mpito.
Pia aliisifu kwa kuwa na mtindo wa kusuluhisha migogoro kwa mazungumzo na mashauriano, wala sio kwa njia ya ghasia.
Alisema kuwa Afrika kama bara limepiga hatua kubwa upande wa demokrasia katika miaka ya hivi karibuni.
Obama atazuru Afrika Kusini ambako rais mstaafu Nelson Mandela anaugua sana na amelazwa hospitalini.
Aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanamuombea Mandela pamoja na familia yake.
BBC Swahili
Rais Barack Obama (kushoto) na rais wa Senegal Macky Sall wakipeana mikono mara baada ya kuongea na wandishi wa habari rais Obama akiwa katika ziara ya kutembelea nchi za Senegal, Africa ya kusini na Tanzania
Wananchi wa wa Senegal wakiwa barabarani wakimsubiri rais Obama pamoja na rais wa senegal Sall wakiwa mitaa ya huko leo
Rais Baraka Obama akiwapungia baadhi ya watu waliokuja kumsikiliza wakati akiongea na wandishi wa habari leo nchini Senegal kulia ni rais Macky Sall mkutano uliofanyika katika jengo la ukulu ya Dakar,
0 maoni:
Post a Comment