Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

ALHAJ MWINYI: FUNDISHENI SAYANSI KWA KISWAHILI

Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akisisitiza jambo wakati akifungua Maonyesho ya 5 ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com).

Mkurugenzi Mtendaji wa Young Scientists Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha akimtambulisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa Balozi wa Kenya nchini Tanzania Chirau Ali Mwakwere kabla ya kufungua maonyesho hayo mwishoni mwa wiki.

Na Daniel Mbega wa brotherdanny.com

RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, amewataka walimu katika shule za msingi na sekondari kutumia lugha ya Kiswahili kufundisha sayansi, kwani lugha hiyo inaeleweka vizuri.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Tano ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini jijini Dar es Salaam jana, Alhaj Mwinyi amesema Kiswahilini lugha inayoeleweka vizuri, si kwa wanafunzi tu,bali hata kwa watu wengine, hivyo ni vyema walimu wakaweka mkazo katika kuitumia kwenye masomo ya sayansi.

“Nimepita kwenye maonyesho haya, baadhi ya wanafunzi walikuwa wananiuliza ‘tukueleze kwa Kiswahili au kwa Kiingereza’, nikasema tumieni lugha yoyote tu. Wengine wamenieleza Kiingereza na wengine Kiswahili.

Balozi wa Kenya nchini, Chirau AliMwakwere (wa pili kushoto) na Balozi wa Ireland nchini, Fionnuala Gilsenan wakisikiliza kwa makini maelezo ya wanafunzi walioshiriki maonyesho hayo. Nyumaya Balozi Gilsenan ni Dk. Gosbert Kamugisha, Mkurugenzi Mtendaji wa Young Scientists Tanzania.

Mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonyesho hayo, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi (katikati) akifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa utuaji wa tuzo. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa YST, Prof. Eligius Lyamuya. Wengine ni Balozi wa Ireland nchini, Fionnuala Gilsenan na Balozi wa Kenya nchini, Chirau Ali Mwakwere.

“Lakini nataka niwaambie, walionieleza kwa Kiswahili, pamoja na utafiti wao kuwa katika lugha ya Kiingereza, walifafanua vizuri sana na nikasema ‘aah, kumbe Kiswahili kinaweza kutumika kufundisha vizuri sayansi,” alisema.

Aliongeza kusema kwamba, yeye wakati anaingia darasa la tano, mwalimu wake wa sayansi alikuwa rais wa Scotland, lakini alimfundisha sayansi kwa Kiswahilina ndio msingi wake mkubwa wa kulifahamu vyema somo la sayansi.

Akizungumzia maonyesho hayo yaliyoandaliwa na kuratibiwa na taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST), Alhaj Mwinyi amesema ni jitihada nzuri za kuandaa wataalam wa kesho katika sayansi.

Maonyesho hayo yalifanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee yakishirikisha jumla ya wanafunzi 240na walimu 120 kutoka shule 120 nchini.

“Hii inafurahisha kuona watoto wadogo wanaichambua sayansi kwa kufanya tafiti hizi nzuri kabisa na kwa hakika nawapongeza sana waandaaji na muendelee hivyo hivyo kuandaa kizazi cha sayansi,” alisema Alhaj Mwinyi.

Wadhamini wakuu wa maonyesho hayo, Kampuni ya BG Tanzania, wamesema wataendelea kudhamini maonyesho yajayo ili kuweka hazina ya wataalamu wa sayansi wa kesho.

“Sisi tunajihusisha na utafiti wa gesi na mafuta, tunahitaji wanasayansi wataalamu ambao lazima tuanze kuwekeza sasa, ndiyo maana katika maonyesho ya mwaka huu tumetoa Dola 200,000 na mwakani tutatoa kiasi kingine ambacho kinaweza kuwa kama hicho au zaidi,” alisema Makamu Rais wa BG Tanzania, John Ulanga, ambaye anayeshughulikia Sera na Masuala ya Uhusiano.

Naye Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Fionnuala Gilsenan, ambao ni wadhamini wa maonyesho hayo, alisema nchi yake itaendelea kuunga mkono jitihada za YST kama ambavyo wamekuwa wakifanya tangu maonyesho hayo yalipoanza mwaka 2011.

Katika maonyesho hayo ya tano, wanafunzi wa Mzumbe Sekondari kutoka Morogoro, Edwin Luguku na John Method, ndio walioibuka washindi wa jumla kutokana na utafiti wao usemao “Kupunguza Matumizi ya Mifuko ya Plastiki Tanzania” (Reducing The Use of Plastic Bags in Tanzania).

Kwa ushindi huo, vijana hao ambao mbali ya kupata medali na tuzo na wamepata zawadi ya hundi ya Shs. 1 milioni. Walikabidhiwa zawadi zao na Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

Washindi wa pili walikuwa Emmanuel Lemalali na Emmanuel Sanga kutoka Tanga Technical na utafiti wao wa ‘A Simple Method For Controlling Ecto-parasites’, ambao wamepata medali na tuzo pamoja na hundi ya Shs. 1 milioni, ambapo walikabidhiwa zawadi zao na Balozi wa Ireland nchini, Fionnuala Gilsenan.

Zawadi nyingine kwa washiriki wa maonyesho hayo zilikuwa katika makundi manne ambayo ni Sayansi ya Baolojia na Ikolojia (Biological and Ecological Sciences) iliyodhaminiwa na Taasisi ya Afya Ifaraka; Sayansi ya Kemikali, Hisabati na Fizikia (Chemical, Mathematical and Physical Sciences) iliyodhaminiwa na Taasisi ya Fizikia (Institute of Physics); Sayansi ya Kijamii na Kitabia (Social and Behavioural Sciences) iliyodhaminiwa na shirika la Concern; na Teknolojia (Technology) iliyodhaminiwa na Karimjee Jivanjee Foundation.

Katika makundi hayo, mbali ya kupatiwa medali na tuzo, washindi wa kwanza walipata Shs. 500,000, washindi wa pili Shs. 300,000 na washindi wa tatu Shs. 200,000.

Aidha, wadhamini wengine wa maonyesho hayo walitoa zawadi mbalimbali ambao ni Songas, Read International, Solaris, Spicenet, Karimjee Jivanjee, Masumin Printways,  First Car Rental, Vernier, na Human Development Innovation Fund (HDIF).

Washindi wa tuzo maalum:

Tuzo ya Kupenda Sayansi ya Songas: Venance Msechu na Martin Oisso kutoka St. Jude Sekondari, Arusha na utafiti wao ‘Automatic House Control System’.

Tuzo ya Read International: Evance Marumbwe na Sara Ismail kutoka Mtapika Sekondari, Mtwara na andiko lao la ‘Mbinu za Ufundishaji Zinachochea Kukua kwa Taaluma (Do Teaching Methods Influence Academic Performance?)

Tuzo ya Solaris: Emmanuel Lemalali na Emmanuel Sanga kutoka Tanga Technical na utafiti wao wa ‘A Simple Method For Controlling Ecto-parasites’.

Tuzo ya Masumin Printways: Maregesi Nyamajeje na Peter Kailembo kutoka Mwasele Sekondari, Shinyanga na andiko lao la ‘Designing a Temperature Sensor’.

Tuzo ya First Car Rental: Augustino Simon na Felister Stanley kutoka Butimba Day, Mwanza na utafiti wao wa Who Votes In Mwanza? (Nani Anayepiga Kura Mwanza?).

Tuzo ya Vernier: Tunu Ngajilo na Ally Salum kutoka Mbeya Sekondari na utafiti wao wa Automatic Irrigation System.

Tuzo ya HDIF: Tunu Ngajilo na Ally Salum kutoka Mbeya Sekondari na utafiti wao wa Automatic Irrigation System.

Tuzo ya Spicenet: Geofrey Ndunguru na Yusuph Mwenda, Songea Boys, na utafiti wao wa Analysis of Blind Students Attitude Towards Science (Uchambuzi wa Hulka ya Wanafunzi Wasioona Katika Mwelekeo wa Sayansi).

Washindi wa makundi mbalimbali:

Sayansi ya Baolojia na Ikolojia:

1. Mariam Ngaula na Latifa Mussa kutoka Kilakala Sekondari, Morogoro na utafiti wao wa ‘The Scarcity of Water in Morogoro’.

2. Saada Abeid na Zaina Maliki wa Mtwara Girls na utafiti wao wa ‘Leaching effects for Maize growing In Mtwara’.

3. Latifa Hamad Ali na Salma Hussein Haji kutoka Kiembe Samaki Sekondari, Zanzibar na utafiti wao wa ‘Exploring Lippia Asperifolia Leaves (Mpambaake) On Anaemic Pregnant Women’.

Sayansi ya Kemikali, Hisabati na Fizikia:

1. Adil Abdallah na Kevin James kutoka Loyola Sekondari, Dar es Salaam na utafiti wao wa ‘Micro Plastics In Drinking Water’.

2. Maryam Salim na Betty Pentzel kutoka Popatlal Sekondari, Tanga na utafiti wao wa ‘The Effects Of Chemical Hair Products And Its Solution’.

3. Patrick Boniface na Jacob John kutoka Mara Sekondari na utafiti wao wa ‘First Principle Of Integration’.

Sayansi ya Kijamii na Kitabia:

1. Latifa Mohamed na Raphael F. Nyamhanga wa Mtwara Technical na utafiti wao wa ‘Is ICT the solution to poor academic performance?’

2. Nancy George na Christermine Christopher kutoka Debrabant Sekondari, Dar es Salaam na utafiti wao wa How To Reduce Road Accidents In Kilwa Road (Jinsi ya Kupunguza Ajali za Barabarani Katika Barabara ya Kilwa).

3. Aloyce Botto na Devis Mafuru wa Tumbi Sekondari, Kibahana utafiti wao wa ‘Swahili Language As A Medium For Learning And Instructions In Tanzania’.

Teknolojia:

1. Venance Msechu na Martin Oisso kutoka St. Jude Sekondari, Arusha na utafiti wao ‘Automatic House Control System’.

2. Tunu Ngajilo na Ally Salum kutoka Mbeya Sekondari na utafiti wao wa Automatic Irrigation System.

3. Salivius Simon na Derick Deusdedit kutoka St. Joseph Kolping Sekondari na utafiti wao wa ‘Carrying Capacity Governing Device’.

Tuzo ya Karimjee Jivanjee:

Washindi ambao watafadhiliwa masomo ya shahada ya kwanza chuo kikuu ni Petro Samson Ndegeleki na Juma Joshua Wiliam kutoka Nassa Sekondari ambao utafiti wao ulihusu ‘How Different Natural Fertilizers Affect the Growth Of Maize’. Washindi hao pia watagharamiwa safari ya kwenda Dublin, Ireland kuhudhuria maonyesho ya sayansi ya BT YSTE Januari 2016.

Washindi wa Pili wa jumla:

Emmanuel Lemalali na Emmanuel Sanga kutoka Tanga Technical na utafiti wao wa ‘A Simple Method For Controlling Ecto-parasites’.

Washindi wa Jumla 2015:

Edwin Luguku na John Method wa Mzumbe Sekondari na andiko lao la ‘Reducing the use of plastic bags in Tanzania’.

(Imeandaliwa na www.brotherdanny.com)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO