Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja na Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam John Guninita Watangaza Kuhama CCM na Kujiunga Rasmi na CHADEMA Leo

post-feature-image

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja ametangaza Kuhama CCM na Kujiunga Rasmi na CHADEMA Leo

 

Aliyekuwa Mwenyekiti -CCM mkoa wa Dar es Salaam John Guninita

---

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja na aliyekuwa mwenyekiti mkoa wa Dar es Salaam John Guninita wametangaza leo kuachana na CCM na kujiunga Chadema.

Makada hao wa CCM wametangaza kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam leo.

Wakizungumza katika mkutano huo, makada hao wamesema wamechukua uamuzi huo baada ya kubaini CCM imepoteza mwelekeo na kwamba kinaendeshwa kibabe tofauti na misingi ya kuasisiwa kwake.

Wametolea mfano wa kukiukwa kwa demokrasia kulikofanywa wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea urais wa chama hicho ambapo Dr John Magufuli aliteuliwa kupeperusha bendera ya CCM.

Hatua ya makada hao imekuja ikiwa ni siku moja tu tangu aliyekuwa mbunge wa chama hicho jimbo la Sikonge, Said Nkumba atangaze kuachana na chama hicho na kujiunga na Chadema.

Huo ni mwendelezo wa matukio ya makada na wabunge chama hicho kuhamia upinzani hasa Chadema kwani awali aliyekuwa waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliachana na CCM baada ya jina lake kukatwa na kamati ya maadili ya chama hicho.

Wengine waliohama CCM ni aliyekuwa mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye, aliyekuwa mbunge wa Segerea, Makongoro Mahanga ambaye pia ni naibu waziri Kazi na Ajira, aliyekuwa mbunge wa Kahama, James Lembeli, aliyekuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM, Mgana Msindai na mbunge wa viti maalumu anayemaliza muda wake Esther Bulaya

CHANZO: HAKI NGOWI .COM

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO