Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

UFAFANUZI KWA KUHUSU KASORO ZA BVR NA UWEKAJI WAZI WA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) ulikamilika tarehe 04/08/2015 katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.

Baada ya kukamilika kwa zoezi la Uboreshaji Tume imekuwa ikichakata (processing) taarifa za Wapiga Kura ili kuweza kuandaa Daftari la Awali la Wapiga Kura, katika maandalizi hayo mifumo imeweza kugundua kasoro mbali mbali ambazo baadhi zimefanyiwa kazi na zingine zinaendelea kufanyiwa kazi, kasoro hizo ni pamoja na Wapiga Kura Kujiandikisha zaidi ya mara moja.


Mfumo wa BVR unao mfumo mdogo wa “Mini AFIS” unaoweza kubaini Mpiga Kura anayataka kujiandikisha zaidi ya mara moja katika kituo husika, mfumo huo ulikuwa umeandaliwa ili kuweza kubaini Wapiga Kura wanaotaka kujiandikisha zaidi ya mara moja na kuzuia Uandikishaji huo katika BVR Kit yoyote.


Hii ingewekana iwapo Mfumo wa mawasiliano ungekuwa na nguvu katika vituo vyote na kuweza kuwasiliana na mifumo iliyoko katika kituo kikuu cha maandalizi ya Daftari(Data Processing Center) kwani katika kituo hicho imewekwa mifumo ya hali ya juu inayoongoza kimataifa katika kulinganisha alama za vidole na kubaini waliojiandikisha zaidi ya mara moja.


Kwa kutokuwa na mawasiliano yenye nguvu kutoka katika kila kituo Tume ilianza kulinganisha taarifa za Wapiga Kura mara tu baada ya taarifa kufikishwa katika kituo cha maandalizi ya Daftari hivyo kwa mitambo iliyopo Tume imebaini Wapiga Kura wote waliojiandikisha Zaidi ya mara moja ambao taarifa zao zimeisha chakatwa ambao kwa sasa imefikia 52,062 Idadi hii inaweza kuongezeka au kupungua kulingana na uchakataji wa taarifa.


Baadhi ya vituo kutokuwa na Wapiga kura.


Tatizo hili linasababishwa na maombi ya kuanzishwa kwa vituo wakati zoezi la Uandikishaji limeanza, baadhi ya vituo hivyo havikutumika wakati wa Uandikishaji kama ilivyokusudiwa kwa sasa Tume inafanyika kazi ya kuhamisha Wapiga Kura na kuwapeleka katika vituo hivyo ili kuwapunguzia umbali mrefu kutoka kwenye vituo walivyojiandikisha wakati wa zoezi la Uandikishaji, kazi hii Tume inaendelea kuifanya kwa kushirikiana na watendaji wa Kata katika Halmashauri husika.


Baadhi ya Vituo kuwa na Wapiga Kura wachache au Wengi katika Vituo vya Uandikishaji.


Tatizo hili pia lilisababishwa na vituo kuongezwa wakati zoezi la Uandikishaji limeanza. Kabla ya kuongezwa vituo katika BVR kutokana na hamasa ya Wapiga Kura Kujiandikisha Wapiga Kura hao walianza kujiandikisha katika vituo vingine na baada ya kuongeza vituo katika BVR vituo vilivyoongezwa viliendelea kufanya Uandikishaji kwa siku mbili au tatu za mwisho hivyo kuonekana kama vina Wapiga Kura wachache, kasoro hiyo inarekebishwa pia kwa kusaidiana na watendaji wa Kata husika ili kuwahamisha Wapiga Kura waliojiandikisha katika vituo kabla ya kuongeza kwenye BVR vituo vilivyoombwa kuongezwa na kupelekwa kwenye vituo karibu na maeneo wanayoishi.


Wapiga kura kuandikishiwa katika Mfumo wa Mafunzo.

Katika taarifa zilizochakatwa imebainika kuwa baadhi ya Wapiga Kura waliandikishwa kwa kutumia mfumo wa mafunzo uliowekwa katika katika BVR kit iliyotakiwa kutumika wakati wa mafunzo tu, Usahihi wa taarifa za Biometric za Wapiga Kura hao kuwa sahihi lakini baadhi ya taarifa nyingine kuhitaji marekebisho kutoka katika fomu za Uandikishaji zilikizojazwa. Kazi hiyo inaendelea kufanyika katika kitu cha maandalizi ya Daftari kwa kuwa fomu zote za uandikishaji zimeishafika.


Marekebisho hayo yalichelewesha kidogo baadhi ya taarifa katika madaftari yaliyowekwa wazi. Kazi ya Kurekebisha kasoro hizo zimeendelea kurekebishjwa na kabla ya tarehe 05/09/2015 kasoro zote zitakuwa zimerekebishwa.


Baadhi ya Taarifa za Wapiga Kura kutochukuliwa taarifa zao katika BVR Kit.

Tatizo hili lilisababisha baadhi Wapiga kura kutoonekana katika vituo walivyojiandikisha, zipo baadhi ya BVR Kit ziliibiwa na zikafanyika jitihada za kung’oa baadhi ya vifaa katika BVR kama vile Laptop na vifaa vingine.


Zipo BVR mbili (2) kati ya BVR Kit 8000 ziliibiwa na walioiba walifanya jitihada za kuiba baadhi ya vifaa katika BVR kit hizo, BVR Kit hizo zilipatikana lakini zikiwa katika hali mbaya ya Uaribifu hivyo kushidwa kuondoa taarifa za Wapiga Kura mara moja, kwa kuwa Tume iliweka vifaa mahususi inapojitokeza changamoto kama hiyo kutopoteza taarifa za Wapiga Kura, chombo hicho kinachohifadhi taarifa za Wapiga Kura mara inapotokea uaribifu mbukbwa hususan wa kompyuta kuweza kupata taarifa za Wapiga Kura bila tatizo, Tume tayari imekwisha pata vifaa vilivyokuwa vimeifadhi taarifa za Wapiga kura na tayari taarifa hizo zinaingizwa katika mfumo wa kuchakata taarifa za Wapiga Kura.

Kata Mpya.


Kwa mujibu wa sheria OWM ­ TAMISEMI ndiyo yenye hadhi ya kupandisha na kugawa maeneo ya kiutawala ili kuchochea maendeleo ya haraka kwa wananchi wake. Mabadiliko hayo ya mipaka ya kiutawala yanahitaji kuhuishwa na Tume katika Mifumo yake ili kuwezesha chaguzi kufanyika na hasa chaguzi za madiwani, hivyo yanafanyika marekebisho ya kuhamisha kuweka vituo na Wapiga Kura katika maeneo mapya ya kiutawala yaliyoanzishwa, ikiwa ni pamoja na:­ Vitongoji, Mitaa,Vijiji, Kata na Halmashauri.


Baadhi ya Taarifa za Wapiga Kura taarifa zao kukosewa na BVR Kit Opereta wakati wa Uandikishaji.


Baadhi ya Wapiga kura taarifa zao zilikosewa na BVR Opereta wakati wa Uandikishaji hivyo kuhitaji marekesho na kupatiwa kadi mpya. Tume ilipeleka BVR Kit katika Halmashauri zote wakati wa kuweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura, ili kufanya marekebisho ya taarifa za Wapiga kura pale panapohitajika. Marekebisho yamefanyika Tume inategemea Taarifa hizo zitafika na kuingizwa katika mifumo ili kupata taarifa sahihi.


Wapiga Kura Kujiandikishia katika maeneo tofauti na maneo wanayoishi.

Baadhi ya Wapiga Kura walijiandikisha katika maeneo tafauti na maeneo wanyaoishi, hivyo kuhitaji kuhamisha taarifa zao, tatizo hili limebainika katika maeneo mengi ya mjini, hasa kwa Wapiga Kura kutaka kuwahi kupata kadi za Mpiga kura, kasoro hii imeendelea kurekebishwa wakati wa zoezi la kuweka wazi Daftari.


Uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura.

Uwekaji wazi wa Daftari la awali la Wapiga Kura ni takwa la kisheria, kifungu cha 11a cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 kinaitaka Tume kuweka wazi Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uhakiki wa Taarifa na kurekebisha kasoro zozote zinalizojitokeza.


Ili kuhakiki taarifa katika Daftari la Awali la Wapiga Kura wananchi wanatakiwa kufika katika Ofisi za kata ili kuweza kuangalia kama majina yao yapo katika Daftari, na ikiwa Taarifa zao ni sahihi mfano Jina, Jinsia, Tarehe ya kuzaliwa na Kituo chake cha kujiandikishia, Aidha, kwa Wapiga kura waliohama kata au jimbo moja kwenda kata au jimbo lingine wanatakiwa kuhamisha taarifa zao.


Zoezi hili la uhakiki lilianza rasmi tarehe 07/08/2015 katika Mikoa mbali mbali na limekuwa likiendelea hadi sasa ili kuhakikisha kila Mpiga kura aliyeandikishwa kupiga kura anaweza kupiga kura bila usumbufu wowote.


Katika zoezi hili Tume imeweka utaratibu wa kuwaondoa watu wote waliojiandikisha katika Daftari ambao siyo raia wa Tanzania, ambapo mchakato huo unaishia katika mahakama ya wilaya.


Ili kasoro hii iweze kuondolewa Tume inahitaji kwa kiasi kikubwa Ushirikiano na wananchi wanaoishi nao ili kuwawekea pingamizi na waweze kuondolewa katika Daftari, ni ukweli kwamba iwapo wananchi watawaficha na kutowawekea pingamizi tatizo hili litakuwa gumu kwa Tume kulitatua.


Kasoro mbalimbali zilizobainika wakati wa Uandikishaji Tume itahakikisha inazirekebisha ili kuhakikisha kuwa Tume inakuwa na Daftari sahihi na la kuhaminika.

Imetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi

 

CREDIT: G SENGO

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO