Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MGOMBE MWENZA WA CCM MAMA SAMIA KATIKA KATIKA MAJIMBO YA MONDULI NA LONGIDO MKOANI ARUSHA

 

Wananchi wakiwa wamejawa hamasa kwa nyimbo na nderemo wakati Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassam, alipowasili kwenye Uwanja wa mkutano wa kampeni za CCM leo, katika jimbo la Monduli mkoani Arusha.

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassa, akiwa na Kina mama wa Jamii ya Kimasai, baada ya kuwasii kwenye uwanja a mkutano wa hadhara, eneo Namanga, Longido mkoani Arusha, leo

Mbunge wa Longido anayemaliza muda wake, Lekule Laizer akihutubia kabla ya mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, kwenye uwanja a mkutano wa hadhara, eneo Namanga, Longido mkoani Arusha, leo

  Mgombea jimbo la Longido kwa tiketi ya CCM, Dk. Steven Lumomo (kushoto), akisalimia wananchi baada ya kutambulishwa na Mbunge wa jimbo hilo anayemaliza mda wake, Lekule Laizer, katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika jimbo hilo leo

  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassa, akihutubia wananchi wa kwenye uwanja wa mkutano wa kampeni, eneo Namanga, Longido mkoani Arusha, leo


Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, akiwasikiliza kina mama waiokuwa wakichota maji katika eneo la mtaa wa madukani, Longido mkoani Arusha.

Kijana akishangilia wakati mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili eneo la Madukani, Longido mkoani Arusha leo kuhutubia mkutano wa kampeni.

Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi, akimtambulisha mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, aliyehamia Chadema, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan kwenye Uwanja wa Madukani, Longido mkoani Arusha leo

Mbunge anayemaliza mda wake, katika jimbo la Longido, Lekule Laizer, akimnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo, Dk. Steven Lemomo katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Madukani, Longido mkoani Arusha leo.

Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika eneo la madukani, Longido mkoani Arusha

Mbunge wa Afrika Mashariki, Angela Kizigha (kulia) akizungumza na Kina Mama wa Jamii ya Kimaai baada ya mkutano wa Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, uliofanyika eneo la madukani, Longido mkoani Arusha

"MWAKA HUU MTAISOMA NAMBA" Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani akimwambia Mgombea Udiwani wa Chadema, Anna Oloiwa, aliyefika kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza huyo, uliofanyika eneo la Madukani, Longido mkoani Arusha leo

Kina mama na mabinti wa jamii ya kimasai wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu uliofanyika jimbo la Monduli, mkoani Arusha leo

Wananchi wakijimwayamwaya kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu uliofanyika jimbo la Monduli, mkoani Arusha leo

Aliyekuwa ameomba kugombea Ubunge jimbo la Monduli lakini kura zake zikawa hazikutosha, Mchungaji Amani Silanga, akionyesha aina mbili tofauti za Kadi za Chadema, wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan leo katika jimbo hilo mkoani Arusha. Amani amedai kuwa wakati Chadema kadi ya kwanza ya Chadema ilikuwa ya  rangi ya bluu na nyeusi tu, lakini miaka kadhaa baadaye ilibadilishwa na kuchanganywa na rangi nyekundu baada ya kulazimishwa na Chama cha Freemason cha uingereza ili chama hicho kupatiwa fedha.

Wananchi wa jimbo la Monduli wakiinua mikono kula kiapo cha kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dk. John Magufuli na mgombea Ubunge wa jimbo hilo Melock Sokoine, katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Hiyo ilikuwa kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan.

Sasa na mimi nitaitwa Samia Ole Suluhu" alisema mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika vazi la Kimasai baada ya kuzawadiwa na Kina Mama wa kabila hilo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Monduli mkoani Arusha.

Mgombea Ubunge jimbo la Monduli kwa tiketi ya CCM, Melok Sokoine akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan uliofanyika kwenye jimbo hilo leo

Wagombea wa Udiwani katika kata mbalimbali jimbo la Monduli wakiinua mikono kusalimia wananchi walipotambulishwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo mkoani Arusha leo

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wake wa Kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Monduli mkoani Arusha leo

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwaaga wananchi baada ya kuhutubia  mkutano wake wa Kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Monduli mkoani Arusha leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO