Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: UZINDUZI WA KAMPENI ZA UBUNGE NA UDIWANI JIMBO LA MAGU MKOANI MWANZA.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, akimkabidhi mbele ya wananchi mgombea Ubunge wa Jimbo la Magu, Boneventura Kiswaga, Ilani ya uchaguzi ya 2015/2020 atakayoisimamia katika kuwaletea maendeleo wananchi wa jimboni humo.Picha Na Peter Fabian.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, akimkabidhi mbele ya wananchi mgombea Ubunge wa Jimbo la Magu, Boneventura Kiswaga, Ilani ya uchaguzi ya 2015/2020 atakayoisimamia katika kuwaletea maendeleo wananchi wa jimboni humo.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Magu mkoani Mwanza, Bonevetruta Kiswaga akiwaomba wananchi wamchague kuwa mwakilishi wao katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana katika Uwanja wa mpira Magu mjini waliofurika kumsikiliza akinadi sera zake.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Magu, Bonevetura Kiswaga.

NA PETER FABIAN,MAGU.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza kimeomba radhi kwa wananchi wa Jimbo la Magu mkoani humo kukichagua ili kumaliza kabisa kero na matatizo ya maji safi katika Mji wa Magu na maeneo yanayokabiliwa na changamoto hiyo.

Akihutubia mamia ya wananchi waliofurika katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge na Udiwani jimboni humo jana uliofanyika katika uwanja wa mpira wa mjini Magu, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, alisema kwamba tatizo hilo linashughulikiwa na serikali na liko katika hatua nzuri ya kupunguza maumivu ya uhaba wa maji safi.

Mtaturu aliwaeleza wananchi kwamba kumekuwa na kero ya muda murefu ya upungufu wa maji safi na kusababisha kuwepo changamoto kubwa ya kuhangaika kupata huduma ya maji safi katika mitaa, vitongoji na vijiji vya mji wa magu.

“Tumeikumbusha serikali kwa mara kadhaa na kukubali kuweka bajeti ya kujenga mradi mkubwa wa maji safi kutoka Ziwa Victoria ambao utaweza kuhudumia Mji huu na maeneo mengine ambao utanaraji kuanza kujengwa mwishoni mwa mwaka huu baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu na kutangwazwa kwa zabuni ili kumpata Mkandarasi,”alisema.

Katibu huyo aliwaomba wananchi kuwachagua Bonaventura Kiswaga kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kutokana na kufanya kazi zinazoonekana akiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo aliyemaliza muda waka ili aweze kusimamia na kupigania maendeleo ya jimbo hilo lakini pia kusimamia Ilani ya CCM na kushughulikia kero hiyo ya maji safi na zingine za kijamii.

“Kuna mambo mengi yamefanyika kwenye uwakilishi wa Dk Festus Limbu, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hili ambaye hakugombea tena na kuviacha sasa tunahitaji mtu mwenye upeo, umakini na weredi wa kuyapigania na kusimamia ili kuhakikisha wananchi wanapata ufumbuzi wa haraka ikiwemo kupata huduma za kimaendeleo na kiuchumi kupitia sekta zote,”alisema.

Naye mgombea Ubunge wa Jimbo la Magu, Kiswaga aliwaomba wananchi kumchagua kuwa mwakilishi wao na kipaumbele chake cha kwanza ni kumaliza kero ya maji safi na salama katika Miji wa Magu na maeneo ya vitongoji na vijiji vyenye kukabiliwa na changamoto hiyo pamoja na kuwepo juhudi za kupunguza makali hayo kutokana na ongezeko la watumiaji huku miundombinu ikiwa siyo rafiki kwa wakati huu.

Aidha aliongeza kuwa akiwa mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ameacha mpango kabambe wa wa kutekeleza mradi wa dhalula wa maji safi ambao utawafanya wananchi kutotumia kiasi kikubwa cha fedha kupata huduma hiyo na kudai kuwa utakamilika mwishoni mwa mwezi Novemba wakati serikali kupitia Wizara chini ya usimamisi wa Mamlaka ya Maji safi na Mazingira ya Jijijni Mwanza (MWAUWASA) ikiendelea na utaratibu wa kujenga mradi mkubwa utakaokidhi mahitaji ya wananchi wa mji na vijiji.

Kiswaga aliwaeleza wananchi waliofurika kumsikiliza endapo watampatia lidhaa ya kuwa Mbunge wao, alisema kwamba kipaumbele cha pili kitakuwa ni sekta ya Afya kwa kuhakikisha anasimamia ujenzi wa Vituo ya Afya kila Kata ikiwemo nyumba za watumishi ili kuwezesha kutoa huduma kwa wananchi kama inavyokusudiwa na serikali ikiwemo ujenzi wa barabara za changalawe na lami ikiwemo barabara ya Magu-Ngudu kwa kiwango cha lami.

“Ntahakikisha suala la Elimu linapata msukumo mkubwa kwa kusimamia ujenzi wa vymba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari ikiwa ni pamoja na juenzi wa nyumba za walimu pamoja na kuongeza Sekondari za kidato cha tano na sita (Haigh School), kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madawati na thamani za maabara tulizojenga kwenye kila sekondari ya Kata,”alisema.

Kiswaga awaliwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais Dkt John Magufuri, yeye na Madiwani wote walioteuliwa na CCM kupeperusha bendera ili kuwezesha Ilani ya uchaguzi ya 2015/2020 inatekelezwa kikamilifu na wananchi wapate huduma zinazohitajika katika Sekta za Elimu, Afya, Barabara, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Ajira na Uchumi ili kupiga hatua ya maendeleo

CREDIT: G SENGO

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO