Balozi Mdogo wa China nchini, Zhang Biao akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini China hafla iliyofanyika ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Sycilia Temu wakati wa kuwaaga wanafunzi 78 wanaokwenda kusoma nchini China kwa ufadhili wa nchi ya China jijini Dar es Salaam jana.
Balozi Mdogo wa China nchini, Zhang Biao akizungumza na mwakilishi wa mkuu wa chuo cha Kiislam cha Morogoro,Faraji Tamim katika hafla fupi ya kuwaanga wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini China iliyofanyika ubalozi wa china jijini Dar es Salaam jana.
Mkufunzi wa katika chuo cha Kiislamu cha Morogoro akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo cha Kiislamu cha Morogoro wanaoenda kusoma nchini China.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKAILI imesema kuwa wanafunzi waliopata ufadhili wa kusoma nchini China wameweza kuleta mabadiliko nchini kutokana na kile ambacho wamekipata kutumia katika sehemu mbalimbali za kitaaluma.
Hayo aliyasema Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Sycilia Temu wakati wa kuwaaga wanafunzi 78 wanaokwenda kusoma nchini China kwa ufadhili wa nchi hiyo,amesema waliopata ufadhili wajitume na kuweza kuchangia mabadiliko katika Nyanja mbalimbali ambazo zimewekwa kipaumbele na serikali.
Ufadhili huo katika Chuo cha Kiislam Morogoro (MUM) wanafunzi waliopata ufadhili ni 15 ambapo saba wanachukua uzalmili na saba watasomea Lugha ya Kichina.
Profesa , Sycilia amesema kuwa nchi ya China imepiga hatua kutokana na watu wake kujituma hivyo wanaopata ufadhili wanatakiwa kufanya hivyo na kuweza nchi kukua kiuchumi kutokana na elimu wanayoipata katika nchi hiyo.
Aidha amesema kuwa serikali ya China imekuwa ikitoa kipaumbele katika serikali ya Tanzania kwa kutoa ufadhili hivyo kwa wale wanaopata watumie fursa hiyo kwa kusoma kwa bidii kwani wahitaji wa ndani kutaka kusoma ni wengi.
Kwa upande wa Balozi Mdogo wa China nchini, Zhang Biao wanatambua ushirikiano kati Tanzania na China na kuona kuna umhimu wa kusukuma katika upande wa elimu kusoma na kuweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi kam ilivyofanya nchi yao.
Amesema hadi sasa wametoa ufadhili kwa wanafunzi 1500 katika ngazi ya uzalimili na uzamivu ambapo wataendeleo kufadhili ili kuweza kufikia malengo katika Nyanja mbalimbali.
0 maoni:
Post a Comment