Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa 16 wa mwaka wa Chama Cha Wanasheria wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika SADC uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam leo. (picha na Freddy Maro)
*****
Katika kile ambacho kwa wakati huu kinaweza kuonekana kama kumshtua Rais Kikwete ni hatua yake ya kurejea kauli ambayo imekuwa ikitolewa na viongozi wa Afrika dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kwamba viongozi wengi wa Afrika hawafurahii namna Mahakama hiyo inavyofanya kazi zake kwa kuwashughulikia viongozi wa mataifa ya Afrika. Rais Kikwete alirudia kauli hiyo jana wakati akifungua Mkutano wa 16 wa Wanasheria wa SADC. Mtanzania, Agosti 22, 2015 linaripoti
Hii ni mara ya pili katika muda wa wiki moja Mahakama hiyo inazungumzwa na viongozi wa kubwa wa kisiasa nchini. Mara ya kwanza ilikuwa ni Agosti 15, 2015 Jijini Arusha katika viwanja vya Tindigani-Kimandolu ambapo kulikuwa na mkutano mkubwa wa mgombea wa CHADEMA kwa nafasi ya urais Mh Edward Lowassa akiwakilisha vyama vinavyounda ushirikiano wa kisiasa UKAWA, akitafuta wadhamini aliitahadharisha Serikali kutoendelea kuwatendea visivyo raia wasiokuwa na hatia.
Lowassa alikuwa akizungumzia madhila yaliyoukumba msarafa waka siku moja kabla akielekea msibani na siku hiyo ya mkutano ambapo Polisi walitumia mabomu ya machozi kujaribu kuutawanya msafara wake uliokuwa unatokea KIA kuelekea eneo la mkutano Kimandolu, Arusha.
Akasema alivyokuwa Serikalini alikuwa akisikia tu kuwa wapinzani wanapigwa na Polisi bila sababu lakini sasa amejua. Akaongezea kuwa Serikali ikiendelea na matendo hayo ataandikisha jina lake kwenye Mahakama hiyo ya ICC.
Hatuna uhakika kama maelezo haya ya Lowassa yanauhusiano wowote na kauli ya Rais jana.
Home
HABARI
KIMATAIFA
POLITIKSI
utawala
Rais Kikwete aungana na viongozi wa Afrika kutofurahia Mahakama ya ICC kuwashughulikia waafrika zaidi!
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment