Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WALIYOZUNGUMZA BAADHI YA VIONGOZI KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI ZA URAIS CHADEMA/UKAWA

OTH_0511

 

Katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam jan, kulifanyika Mkutano Mkubwa wa Hadhara ambapo Ilani ya CHADEMA/UKAWA Kwa Uchaguzi Mkuu 2015  na Kampeni zilinduliwa rasmi.  Ilani hiyo ni ya CHADEMA lakini imeridhiwa na vyama vyote vya UKAWA na kuna mapendekezo yao pia yamejumuishwa.

Mwenyekiti Mbowe ndiye aliyetekeleza Tendo la Uzinduzi huo na kuwakabidhi Nakala Wagombea Urasia na Umakamu, Mh Lowassa, Maalim Seif na Babu Duni.

Baadae amewakabidhi pia nakala wagombea Ubunge wa UKAWA kwa Mkoa wa Dar (Mbagala - CUF, Temeke - CUF, Segerea - CUF/CHADEMA, Kawe - CHADEMA, Kibamba - CHADEMA, Ubunge- CHADEMA, Kigamboni - CUF/CHADEMA, Kinondoni - ), kwa niaba ya wabunge wengine. Majimbo ya Kigamboni na Segerea bado hayajapata muafaka. Mbowe alisema Ilani yao ni Rafiki itakayojali wananchi wote wa makundi yote.

OTH_0560
Katika Mkutano huo viongozi mbalimbali walipewa nafasi ya kuzungumza na miongoni mwao ni kama wafuatao.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mh Freeman Mbowe
Mbowe ameungumzia mambo mengi, mojawapo ni haya
Amesema UKAWA ndio wanazindua rasmi kampenzi zao kwa nchi nzima na watazunguka kila kona ya nchi kuhubiri Mabadiliko ambayo amedai sio tu kuitoa CCM Madarakani.

Mbowe amesema mabadiliko wanayoyatamani hayatakuwa na maana kama hayataleta maendeleo kwa watanzania na kurudisha haki nchini. Amesema mabadiliko hayatakuwa na maana kama ustawi wa wananchi hautakuwa jukumu la Serikali.

Mbowe ameenda mbali zaidi na kumjibu Kikwete na Mzee Warioba.
Amemjibu Warioba aliyemsifu Magufuli kuwa ni mzalendo na hana marafiki maatajiri.. Mbowe amemwambia kuwa Umasikini sio sifa ya Uongozi. Wao kama UKAWA wanatamani kila mtanzania awe tajiri aihi maisha bora.

Akamjibu Kikwete pia aliyedai Magufuli ni Mtetezi wa Wanyonge.. Akasema mtetezi hawezi kuwaambia wanyonge wa Kigamboni wasiokuwa na sh 200 wapige mbizi.

Baadae Mbowe akafafanua kwanini wamemkaribisha Lowassa UKAWA
Mbowe anasema walifanya utafiti na kugundua kuwa kuna watu wengi ndani ya CCM wamefungwa minyororo na kwamba Lowassa laikuwa mmoja wao na mhanga wa propaganda na makundi CCM.
Wakajiridhisha kuwa Lowassa anaweza kuwa chachu ya mabadiliko kwa dini zote na makundi yote katika jamii ya Tanzania.

Akihitimisha, aliwashukuru wote waliojiondoa CCM na kudai kuwa Mungu ana njia nyingi za kuzungumza na watu wake na hivyo watanzania watarajie Maisha Mapya na Matumaini mapya.

OTH_0611

Waziri Mkuu wa zamani Serikali ya Mkapa, Mh Fredrick Tluway Sumaye
Sumaye alianza kwa kueleza mshangao wake kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuelezwa kama mfano wa mtu mwenye maadili, akasema “Kama kipimo cha maadili ni Kinana mimi nitakuwa mtakatifu”

Akasema kuwa CCM wamekuwa wakiendesha siasa ya chama kimoja wakiwa wamevaa ngozi ya vyama vingi. Akadai yeye na Lowassa kwa nyakati tofauti walitambua watanzania wanataka mabadiliko tangu jana na walitaka kufanya mabadiliko ndani ya CCM lakini yakawa yale (kukatwa).

Sumaye akasema CCM kuna tatizo kwamba ukitaka kufanya jambo wanakuzunguka. Akadai kuwa wamewajaza watanzania uoaga wa usichokijua (fear of unknown) na kwamba amejiunga UKAWA kuondoa huo uoga wa usilolijua kwa kusaidia ana na Lowassa, UKAWA na wanamabadiliko wengine kufanya maisha ya watanzania yawe bora.  Akawataka watanzania wasirudi nyuma.

Baada ya hapo Sumaye akatumia muda zaidi kufafanua namna mbili ambazo alidai watu wa CCM wanamsakama nazo Lowassa. 
Akasema leo Kikwete anasema Lowassa hafai ilhali alimteua kuwa waziri mkuu wake, na akahoji inawezekanaje Rais amteue mtu ambaye hafai.

Akasema ni Lowassa ndiye aliyefanikisha Kikwete kuingia Ikulu.

Sumaye aakataja maswala manne ambayo alidai hayana mjadala, yako wazi..kwamba watanzania wanampenda Lowassa, kwamba Lowassa ni mchapakazi, kwamba Lowassa anawapenda watanzania na kwamba ndiye atakayeyaleta Mabadiliko.

Baada ya kuongezewa muda, Sumaye akatumia muda huo kufafanua mambo mawili ambayo alidai Lowassa anasemwa nayo sana.
Kwanza, Lowassa ni fisadi na mla rushwa na amechukua hela za matajiri

Sumaye akahoji, kama Lowassa ni mla rushwa, alitoka madarakani mwaka 2008 lakini aliendelea kuwa huru na hakuondoka nchini, kwanini hakujificha na hakushitakiwa!? Akasema Lowassa litumia busara kujiwajibisha ili kumuokoa Rais na Serikali yake.

Baadae akahoji yafuatayo kwamba wakati yanafanyika Lowassa alikuwepo!?
-Kutoroshwa twiga KIA
-Kusamehewa wezi wa EPA
-Madawa ya kulevya kupitishwa JKNIA hadi Afrika Kusini bila kuonekana hadi yanakamatwa huko
-Ununuzi wa vichwa vibovu vya treni
-Ununuzi wa feri chakavu na kudai mpya
-Fidia kwa wajenzi wa barabara kwa kucheleweshewa malipo, kwamba kati ya trilioni moja bilioni 900 ni fedha za adhabu. Akahoji sio ufisadi nao!?
-Ushahidi kuwa Serikali ya Kikwete ni dhaifu sana. AkasemaKatibu Mkuu wa CCM, Kinana alithibitisha kwa kwena hadharani na na kusema Serikali ya chama chake ina mawaziri mizigo.  Akadai kwa nchi zenye demokrasia iliyokomaa Katibu Mkuu wa chama tawala akiwaambia wananchi hayo Serikali inaondoka madarakani kwasababu ni wao ndio waliounda Serikali na kuwateua mawaziri hao na kwamba wananchi hawawezi kumuadhibu waziri, hali aliyodai ni sawa na kusema CCM imeshindwa msiipe kura.
-Sakata la ESCROW, akahoji mgao wa fungu kubwa la Sigh alikula nani maana mgo wa Rugemalira waliokula wanajulikana.

Alivyomaliza hayo, Sumaye akasema CCM wamebaki na kiburi na hawajali tena maumivu ya wananchi..(kwasababu) wanajua watanzania watawapa kura, akadai wasikubali, hawajawahi kuonja mabadiliko ndani ya vyama vingi.

Pili, Lowassa ni mgonjwa
Akifafanua hili, Sumaye alianza kwa kuhoji, kwani Magufuli ni mzima!? Akauliza kama ni wazima wanaenda ulaya kufanya nini!?

Akasema kawaida mtu yeyote aliyefikisha miaka 50 na zaidi hawezi kuwa mzima 100%

Akiongea kwa mtindo wa maswali akahoji.
Kipindi Mkapa akiwa madarakani aliwahi kwenda kufanyiwa operesheni kubwa ulaya na nchi haikuathirika.
Akahoji mbona hata Rais Kikwete alienda Marekani kufanyiwa upasuaji mkubwa wa tezi dume?

Akihitimisha akasema Urais sio kazi ya kubeba zege na kwamba rais anafanya kazi ya kusimamia watendaji wake aliowachagua kama meneja tu, na kwamba Lowassa anaweza.

Akaaga na kudai yuko pamoja na Lowassa, UKAWA na wanamabadiliko wote kuhakikisha CCM inakaa benchi.

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif
Yeye alisalimia tu kwa salamu mpya ya UKAWA (Lowassa…Mabadiliko…Mabadiliko..Lowassa) na kuahidi kuzungumza siku nyingine

Mgombea Mwenza wa Lowassa, Juma Duni Haji
Yeye aliongea mengi lakini makubwa mawili ni kuhusu upatikanaji wa Katiba itokanayo na maoni ya wananchi wakiingia madarakani na kuheshimu kina mama kwa kuboresha upatikanaji wa huduma na mahitaji yao

Waziri wa Mambo ya ndani wa zamani, Mh Lawrence Masha
Ameongea kwa naiaba ya waliowahi kuwa mawaziri na kuelezea mambo mawili
1. Anasema wote waliohama CCM wanaakili timamu na wanajua walichokifanya kwa mujibu wa sheria za nchi, sio makapi
2. Amesema wako askari Polisi wanatumika vibaya. Akasimulia kuwa yeye walimkamata na vijana 19 na kumuweka ndani ili kuwatisha wananchi. Amewataka wananchi wasitetereke, wasiogope.. mabadiliko hayakwepeki ..hakuna wa kuyazuia.

Mwenyekiti wa BAWACHA na mgombea Uunge KAWE, Mh Halima Madee
Wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi kama afya, elimu, uchumi n.k. Amesema wakati ni sasa, imetosha kwa wananwake kuwa wateja wa CCM

Mke wa Lowassa, Mama Regina Lowassa
Amesema anamshukuru sana Mungu, ametenda. Ameahidi kuzungumza na wanawake wote nchini na kujua namna ya kutatua kero zao kupitia Serikali Mpya.

Mwenyekiti wa NLD, Dr Emmanuel Makaidi
Amewaomba wanaYanga na SImba wote wamchague Lowassa na UKAWA kwa ujumla

Mwenyekiti wa CUF
Anasema wale wanaoamini kuwa haiwezekani kupata mabadiliko nje ya CCM, wafute hayo ndani ya ichwa vyao. Mabadiliko yanawezekana nje ya CCM kupitia Lowassa na Timu nzima ya UKAWA. Mabadiliko ni hapahapa.

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na mgombea Ubunge Vunjo, Mh James Mbatia
Mbatia anawatahadharisha Kikwete kuwa asilete Uchochezi nchini. Anasema nchi ni yetu sote.. Anadai Wakati UKAWA wanafanya siasa za kistaarabu na kuheshimu sheria lakini wakuu wa mikoa na wilaya wanakutana Ngurdoto Arusha kupanga hujuma kwenye uchaguzi.
Baadae akanukuu andishi la Biliblia na kuimba utenzi. Mhubiri 4:13 "Heri Masikini wenye Hekima kuliko Mfalme Mzee Mpumbavu ambaye hasikii tena m.."

Tambwe Hiza, aliyewahi kuwa Mkuu wa Kitengo cha Propaganda CCM
Yeye aliungumzia

OTH_0309
PICHA ZOTE NA: OTHMAN MICHUZI

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO