Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

SIKU YA KIMATAIFA YA VIJANA DUNIANI YAADHIMISHWA KWENYE VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR



Maandamano  yakiongozwa na bendi ya jeshi la polisi
 
Baadhi ya vijana kutoka shule mbalimbali wakiandamana kuingia katika viwanja vya mnazi mmoja wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishw  jijini Dar es Salaam. Mashirika mbalimbali  ya mataifa yanayofanya shughuli za vijana ni kamaUNFPA, IYF, UNIC, ILO, RESTLESS DEVELOPMENT, YUNA, AMREF, MARIE STOPES, pamoja na PSI.(Picha zote na Geofrey Adroph)
 
 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na viongozi wengine wakipokea maandamano ya vijana wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi na wapili kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanem.
 
 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja viongozi wengine wakipokea maandamano ya vijana wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
 Viongozi katika meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem akizungumza na vijana wakati wa Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Katika hotuba yake aliweza kuzungumzia maswala ya watoto wa kike kubeba mimba wakiwa na umri mdogo ambao unapelekea kuacha masomo kutokana na ujauzito huo pia aliwasisitiza vijana kuwa na umoja kwani ndio nguvu kazi ya Taifa.
Mwendeshaji wa Sherehe hiyo Bi. Usia Nkhoma ambaye ni Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC)  akizungumza jambo na  vijana walioshiriki maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi(wa nne kutoka kulia) akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na vijana wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Wa tatu kutoka Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, Wa kwanza kulia ni Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum na wa pili kutoka kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem.
 Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akitoa shukrani kwa wawakilishi wa Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum na wa pili kutoka kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem.
Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwahutubia vijana walioshiriki maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake aliwasisitiza vijana kujitokeza katika uchaguzi unaotegemea kufanyoka mwezi wa kumi mwaka huu ili kuchagua viongozi makini watakaoweza kutetea masuala ya vijana na pia aliwasisitiza vijana kufanya kazi za kujitolea.
 Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum akiwasalimia vijana walioshiriki maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Bw. Hesein Melele(wa kwanza kuli) kijana ambaye ni mwakilishi wa asasi ya vijana chini ya umoja wa mataifa (YUNA) akiwasilisha maazimio yaliyofikiwa na vijana wakati wa kongamano lililofanyika Agosti 10 mwaka huu kujadili ujumbe wa siku ya kimataifa ya vijana duniani na kuandaa maazimio yaliyowasilishwa kwa mgeni rasmi leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja walipokua wakiadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani.
 Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, Tatu Ahmed akitoa shukrani kwa wageni waalikwa waliofika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja walipokua wakiadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani.
Mratibu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutoka asasi ya vijana chini ya umoja wa mataifa (YUNA), Rahim Nasser akiwatolea ufafanuzi vijana waliofika kwenye banda la Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani  Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akimsikiliza kwa makini Mratibu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutoka asasi ya vijana chini ya umoja wa mataifa (YUNA), Rahim Nasser alipotembelea kwenye banda la Umoja wa Mataifa
 Mkufunzi wa Ujasiriamali/Biashara wa Program ya anzisha na imarisha biashara yako (SIYB) iliyochini ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), Bw. MacDonald Lanzi (wa pili kutoka kulia) akimfafanulia jambo Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel. Wa pili kushoto ni Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum na wa kwanza kutoka kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem.
Mshauri na Mkufunzi wa Ujasiriamali/Biashara wa Program ya anzisha na imarisha biashara yako (SIYB) iliyochini ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), Bw. Lawrence Ambokile(mwenye koti jeusi) akitoa ufafanuzi kwa Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipotembelea banda ilo
 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akisaini kitabu katika kwenye moja ya bada la PSI Tanzania katika Viwanja vya Mnazi Mmoja walipokua wakiadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani. kushoto ni Dkt. Benedict Nyiro
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem akisaini kitabu katika kwenye moja ya bada la PSI Tanzania katika Viwanja vya Mnazi Mmoja walipokua wakiadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani. kushoto ni Dkt. Benedict Nyiro
 Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum akisaini kitabu katika kwenye moja ya bada la PSI Tanzania katika Viwanja vya Mnazi Mmoja walipokua wakiadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani. kushoto ni Dkt. Benedict Nyiro
Ofisa Habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC), Stella Vuzo(wa kwanza kushoto), Meneja mradi wa ICS Bi. Imisa Masinjila(wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara hiyo Prof. Hermas Mwansoko(wapili kutoka kulia) pamoja na Imisa Masinjila wakizungumza jambo maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum(wa kwanza kushoto) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem(katikati) wakizungumza jambo na  Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi  wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya vijana waliofika kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Bw. Hesein Melele(katikati) kijana ambaye ni mwanachama wa asasi ya vijana chini ya umoja wa mataifa (YUNA) akiwa kwenye picha ya pamoja na vijana wenzake ambao ni Rehema Pascal(kushoto) pamoja na Felister
  
 
 
 
 
 
 
 

 Vijana kutoka vikundi mbalimbali wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 
 
 
Vijana wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO