Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KINANA ASEMA CCM INASHINDANA NA MAKAPI YAKE

 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amesema kwamba chama Chama Mapinduzi kinatarajia kupata ushindi mnono katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwezi oktoba mwaka 2015.

Akizungumza na Wanachama wa CCM leo katika ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es salaam mara baada ya mgombea wake wa Urais Dk.John Pombe Magufuli kuchukua fomu ya kugombea urais tume ya Taifa ya Uchaguzi amesema kwamba chama hicho kwa bahati nzuri mwaka huu kinashindana na makapi yake ambayo kamwe hayawezi kuishinda CCM.

“Nchi yetu inakwenda kwenye uchaguzi ikiwa na wagombea na makapi, sasa kati ya mgombea na makapi nani mshindi?” Amehoji Kinana

Ameongeza kuwa kila mwanachama akitengwa na CCM mahala pake ni wapi? Huku mamia ya wananchi wakijibu ‘Chadema’ kwa sauti ya juu.

Naye Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya Kikwete amesema kwamba serikali ya CCM imefanya mambo mengi ya Maendeleo na mwaka huu wana waahidi watanzania ushindi wa kishindo.


Kwa upande wa Mgombea Urais wa CCM Dk. John Magufuli amesema kwamba ikiwa atachaguliwa kuwa rais anakwenda kufanya wananchi walicho mtuma kwa kuwa shida za watanzania anazifahamu huku akirejea kauli yake Maendeleo hayana chama.


Hivi karibuni chama cha Mapinduzi kimepata mtikisiko mkubwa kufuatia wanachama wake kuhama chama hicho na kutimkia Upinzani hususani Chama cha Chadema akiwemo Waziri mkuu wa Zamani Edward Lowassa, Makongoro Mahanga, James Lembeli pamoja na Este

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO