Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KAMPUNI YA STARTIMES YA ZINDUA BUNDESLIGA

 

Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,  Leonard Thadeo akipiga mpira kuelekea golini kwa mlinda mlango,  Maulid Kitenge ambaye ni mtangazaji wa kituo cha redio cha EFM kuashiria uzinduzi rasmi wa ligi ya Ujerumani, Bundesliga itayorushwa moja kwa moja kupitia ving’amuzi vya StarTimes nchini. Wanaoshuhudia tukio hilo lililofanyika makao makuu ya kampuni hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wa kwanza kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo nchini, Lanfang Liao na mshereheshaji wa uzinduzi huo na mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds FM, Shafii Dauda (mwenye kipaza sauti)

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya StarTimes Tanzania,  Lanfang Liao akipiga mpira kuelekea golini kwa mlinda mlango , Maulid Kitenge ambaye ni mtangazaji wa kituo cha redio cha EFM kuashiria uzinduzi rasmi wa ligi ya Ujerumani, Bundesliga itayorushwa moja kwa moja kupitia ving’amuzi vya kampuni hiyo. Anayeshuhudia tukio hilo lililofanyika makao makuu ya kampuni hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam (katikati) ni mshereheshaji wa uzinduzi huo na mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds FM,  Shafii Dauda.

Wasanii wa tasnia ya filamu nchini au Bongo Movie kutoka kushoto, Odama, Cathy na Davina wakifurahia na kufuatilia hafla fupi ya uzinduzi wa ligi ya Ujerumuni – Bundesliga kupitia StarTimes pekee. Uzinduzi wa ligi hiyo itakayoanza kutimua vumbi Agosti 14, ulifanyika katika viwanja vya makao makuu ya kampuni hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo (katikati) wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Kilabu cha Simba nchini, Geoffrey Nyange Kaburu (kulia),  wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ligi ya Ujerumuni – Bundesliga kupitia StarTimes pekee. Uzinduzi wa ligi hiyo itakayoanza kutimua vumbi Agosti 14, ulifanyika katika viwanja vya makao makuu ya kampuni hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.



Na mwandishi wetu


Wateja na watanzania wanaopenda soka kwa ujumla watapata fursa ya kufaidi mechi zote za ligi ya   Ujerumani almaarufu kama ‘Bundesliga’ kupitia ving’amuzi vyao vya StarTimes.


Hayo yalibainishwa na uongozi wa Kampuni ya StarTimes Tanzania wakati wa hafla fupi ya kutangaza kuonyeshwa kwa ligi hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika makao yake jijini Dar es Salaam.


Akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi huo Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni,  Leonard Thadeo alisema kuwa Bundesliga ni ligi maarufu na inayopendwa duniani na anaipongeza kampuni ya  kitanzania kwa mara ya kwanza kufanikiwa kupata hakimiliki za kuionyesha.


“Ni hatua kubwa waliyoipiga StarTimes kwa kufanikiwa kuionyesha ligi hii kupitia ving’amuzi vyao. Nina imani kubwa kuwa watanzania wengi wanaopenda soka watafurahia zaidi kwani nimeambiwa kuwa zaidi ya mechi 300 zitaonyeshwa moja kwa moja kupitia chaneli zao tofauti.” Alisema Thadeo


“Mbali na wapenda soka kufurahia ligi hii bali pia ni fursa kwa wachezaji wa kwetu nyumbani kuangalia ni kwa namna gani wenzao wanacheza soka la kulipwa. Kwani kupitia wenzetu ambao wamepiga hatua kubwa katika maendeleo ya soka yapo mengi ambayo tunaweza kujifunza na kuboresha ligi yetu,” alisema Thadeo.

“Napenda kutoa wito kwa watanzania kuendelea kuunga mkono juhudi za kampuni za kinyumbani ambazo zinafanya jitihada kubwa katika kutupatia huduma bora kabisa.” alisema


Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya StarTimes nchini,  Lanfang Liao amebainisha kuwa kuja kwa ligi ya Bundesliga ni muendelezo wa uboreshaji wa huduma zao ikiwemo maudhui waliyonayo katika ving’amuzi vyao.


“Leo ninayo furaha kubwa kuwaambia wateja wetu kuwa sasa ni rasmi ligi ya Ujerumani itawajia moja kwa moja kupitia dikoda zenu za StarTimes. Haya ni mafanikio makubwa ambayo tunajivunia katika kuendelea kuhakikisha kuwa watanzania wanaendelea kufurahia huduma za matangazo ya luninga kwa njia ya dijitali kwa gharama nafuu.” alisema  Liao


“Tumeamua kuwaletea habari hii njema wateja wetu kuwa kuanzia tarehe 14 ya mwezi huu watakuwa na fursa wa kuangalia zaidi ya mechi 300 za ligi ya Ujerumani moja kwa moja. Mechi hizo zitaonyeshwa kupitia chaneli za ST Sport 2, ST Sports Premium na TBC2, hivyo kutoa uwanja mpana kwa watazamaji kuchagua mechi za kutazama. ” alisema


Aliendelea kwa kusema kuwa sababu kuu kwa kampuni yake kupata hakimiliki za kuonyesha ligi hii ni kutokana na huduma bora na nafuu wanazozitoa. Kwani wamiliki wa ligi hiyo wanaamini kuwa mamilioni ya waafrika ambao wengi wana vipato vya chini wanaweza kumudu gharama za ving’amuzi vya StarTimes.


“Kampuni yetu inaongozwa na faslafa ya kuhakikisha kuwa kila nyumba ya mtanzania inakuwa na uwezo wa kupata matangazo ya luninga kwa njia ya dijitali kwa gharama nafuu. Na hilo ni dhahiri kupitia gharama za ving’amuzi na vifurushi vyake ambavyo ni vya chini kuliko kampuni yoyote nchini.


Ni jambo ambalo tunajivunia sana na  kwa kuwajali wateja wetu tumetoa ofa kuanzia tarehe 10 mpaka 14 Agosti kwa mteja atayelipia kifurushi chochote basi atapata tena kifurushi hichohicho kwa malipo yaleyale aliyolipia.


Kwa mfano kama utalipia kifurushi cha shilingi 12,000 basi utalipiwa tena kifurushi hichohicho bure kabisa, naomba watanzania wachangamkie ofa hii ya muda mfupi kabla ya kuanza kwa Bundesliga.”

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-0712-727062)

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO