Lowassa na msafara wake wa makumi ya wafuasi wa ushirikiano wa vyama vinne maarufu kama UKAWA wamejikuta wakishindwa kuendelea na safari ya kumsindikiza Mgombea wa Urais kupitia CHADEMA, chama mshirika wa umoja huo Mh Edward Lowassa kuhudhuria sherehe za maziko ya Maehemu Mzee Peter Kisumo na kurejea Mjini Moshi.
Baadhi ya viongozi alioambatana nao Mh Lowassa na wote wamerudi baada ya kuziiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Mh James Mbatia, Mbunge wa Rombo Mh Joseph Selasini, Mbunge aliyemaliza muda wake Moshi Mjini Mh Philemon Ndesamburo na viongozi wa Mkoa na Wilaya.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, tukio hilo limetokea mchana wa leo eneo la Kijiji cha Maroro Wilayani Mwanga ambapo askari wa Jeshi la Polisi kwa kutumia magari yake na rilaha za moto na mabomu ya mwachozi walitanda badarabari kuzuia msafara huo usiweze kuendelea.
Blogu hii haijaweza kupata sababu hasa zilizopelekea Jeshi la Polisi kuamua uamuzi huo kuwazuia watu waliokuwa wnakwenda kwenye msiba wa Mzee Kisumo. Hata hivyo dodoso za hapa na pale zinaeleza tetesi kuwa askari hao wametekeleza tu maagizo ya wakubwa wao.
0 maoni:
Post a Comment