Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MBUNGE WA LUDEWA DEO FILIKUNJOMBE APINGWA KUPITA BILA KUPINGWA MCHAKATO WA UCHAGUZI MKUU

 

Mgombea Ubunge Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Msambichaka Mkinga (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akipinga kupitishwa bila kupingwa mgombea mwenzake wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Deo Filikunjombe na kudai kulikuwa na hujuma. Kulia ni Wakili wake, Paulo Kalomo.

  Mgombea Ubunge Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Msambichaka Mkinga, akionesha fomu namba 10 ambazo alikabidhi kwa Msimamizi wa Uchaguzi.

Wakili wake, Paulo Kalomo, akizungumza katika mkutano huo kuhusu sheria inavyoelekeza.

Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.


Na Dotto Mwaibale

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Msambichaka Mkinga amepinga vikali kupitishwa bila kupingwa mgombea mwenzake wa jimbo hilo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Deo Filikunjombe na kudai kulikuwa na hujuma.

Mkinga alitoa malalamiko hayo mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi na kueleleza kuwa sababu zilizotolewa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo kuwa hakupeleka fomu namba 10 hazikuwa na ukweli wowote.

"Nilipofika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ludewa nilisaini na kukabidhi tamko la kuheshimu na kutekeleza maadili ya uchaguzi ya mwaka 2015 (fomu namba 10) na baada ya kusaini nilimkabidhi msimamizi wa uchaguzi pamoja na fomu namba 8B,picha, stakabadhi ya malipo ya dhamana ambapo vilihakikiwa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Gervas Lupembe" alisema Mkinga.

Mkinga alisema katika jambo lisilo la kawaida msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo hilo hakubandika kwenye ubao wa matangazo tamko hilo na alipomfuata msimamizi huyo kumuulizia msaidizi wake Lupembe alikiri kupokea na kuziwasilisha kwa kiongozi wake ili kutia saini ambaye naye alikiri kuzipokea lakini wakati ana bandika tamko hilo la Mgombea wa CCM fomu hiyo hakuiona.

Alisema katika pingamizi alilowekewa dai mojawapo ni kutokuwepo  tamko hilo kwenye fomu zake hali inayoonesha wazi kuwa kulikuwa na mchezo mchafu uliofanyika ili kumpitisha Filikunjombe bila kupingwa.

Mkinga alisema kuwa kuwaondoa wagombea kwa sababu zisizo za msingi ni kuiminya demokrasia na kuirudisha nchi nyuma kwani kunaweza kusababisha kukosa viongozi wazuri na kubakia na viongozi wasiofaa na wasiotaka kushindanishwa kwa kuwapa nafasi wananchi ya kumchagua kiongozi wanayemtaka.

Mgombea huyo alisema kutokana na sintofahamu hiyo alimuomba msimami wa uchaguzi wa jimbo hilo kutupiliambali pingamizi lililotolewa dhidi yake na mgombea mwenzake ambapo anasubiri majibu baada ya kuandika barua ya malalamiko.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO