Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Wananchi Wamzuia Mgombea Mwenza wa CCM Barabarani Mwanga

IMG_00661 Bi. Samia Othuman Suluhu akipokewa na baadhi ya viongozi na makada wakiwa kwenye mkutano huo.Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo. Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huoMjumbe Mkuu wa Baraza Kuu la Wanawake na Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Same, Anjela Kailuki akizungumza alipokuwa anamnadi Bi. Samia Suluhu,

BAADHI ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamelazimika kuuzuia msafara wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais leo alipokuwa njiani akitokea Wilaya ya Same kuelekea Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro huku wakimuomba awasalimu na kuzungumza nao, kabla ya kuendelea na safari yake. Bi. Samia Suluhu alilazimika kuusimamisha msafara wake baada ya wananchi hao kusogea zaidi barabarani wakati akipita huku wakinyoosha mikono ya kumuomba asimame ili azungumze nao eneo la kilometa chache kabla ya kuingia njia panda. Wananchi hao wengi wakiwa wakinamama walimsimamisha kwa kuingia pembezoni mwa barabara alipokuwa akipita na hivyo kulazimika kusimama kwa dakika chache na kuzungumza nao. Akizungumza aliwaambia amefarijika na kuwaona na mapenzi makubwa na chama chao hivyo kuwaeleza kuwa yeye ni mwanamke pia na anajua kwa karibu kero ambazo wanakabiliana nazo akinamama sehemu mbalimbali na kuahidi endapo watapata ridhaa pamoja na Dk. John Magufuli atahakikisha anasimamia vizuri utaratibu wa kuwawezesha akinamama kupitia vikundi vya kijamii ili waweze kujikwamua kiuchumi pamoja na familia zao. Alisema yeye ni mwanamke mzazi anatambua shida wanazokumbana nazo akinamama hasa kwenye wodi za wazazi hivyo akifanikiwa kuingia madarakani atahakikisha anasimamia ipasavyo ilani ya chama ambayo imeeleza vizuri juu ya uboreshaji huduma za afya ikiwemo wodi za akinamama na hali ya upatikanaji madawa. "...Matatizo ya wanawake nayafahamu vizuri wala sisimuliwi maana na mimi ni mzazi nimeingia wodi ya wazazi mkitupa ridhaa na mwenzangu (mgombea urais, Dk. Magufuli) nitahakikisha nayasimamia haya vizuri," alisema Bi. Suluhu akizungumza muda mfupi na wananchi waliomzuia barabarani wakiomba awasalimu. Alisema kero ya maji imekuwa inawatesa akinamama kwa kutumia muda mwingi kutafuta maji na kushindwa kuzalisha uchumi wa familia ipasavyo, hivyo Serikali ya CCM imeanza mradi wa kutoa maji katika Bwawa la Nyumba ya Mungu na kuyaingiza katika vijiji vyenye shida ya maji. Aidha akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara Mwanga ameisikia kero ya uhaba wa mabweni kwa wanafunzi wa kike suala ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa mabinti hao kutiwa mimba na kukatisha masomo eneo hilo na kudai suala hilo lipo katika ilani ya CCM mwaka huu na litashughulikiwa vizuri endapo watapewa ridhaa na wananchi, ikiwa ni pamoja na suala zima la kupambana na kuongeza fursa za vijana ili kukabiliana na uhaba wa ajira. Alisema Serikali iliyopita imejitahidi kuongeza huduma za umeme katika vijiji ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi lakini katika awamu hii CCM ikipewa ridhaa itahakikisha vijiji vilivyobaki kwa baadhi ya maeneo vinawekewa umeme. Alisema anawapa akinamama kazi kuhakikisha Dk. Magufuli na wagombea wa CCM eneo hilo wanashinda kwa asilimia 80 kwani wao ndio wenye ushawishi mkubwa katika familia. Vivyo hivyo kuwataka madiwani wanaogombea kuhakikisha mgombea uraisi na wengine wanapata kura za kutosha ili kushinda uchaguzi. Kwa upande wake Asumta Mshana aliyekuwa mbunge wa CCM na uchaguzi huu aligombea na kura hazikutosha alisema anawashangaa wanachama ambao waligombea ndani ya Chama Cha Mapinduzi na waliposhindwa wakaamua kuondoka ndani ya chama hicho. Alihoji kwani walipokuwa wakiomba nafasi hizo hawakutambua kuna kushindwa na kushinda? Aliwafananisha wanaofanya hivyo ni sawa na akinababa wanaoamua kukimbia familia zao jambo ambalo ni aibu. "Nawashauri wababi ndani ya chama na kukijenga chama ili kiweze kufanya vizuri, kama kura hazikutosha safari hii usikimbie chama kwani mlikuwa hamjui kuna kushinda na kushindwa unapoomba uongozi," alisema. Naye Mwenyekiti wa CCM, Mkoa Idd Juma Mohamed alimshukuru Bi. Samia kwa kuamua kuanza kampeni katika mkoa wake na kumuhakikishia watahimiza wapiga kura kwani Kilimanjaro bado ni ngome ya CCm na watahakikisha wanatwaa majimbo yote, viti vya udiwani.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO