Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KAMERA YA OTHMAN MICHUZI: YALIYOJIRI UZINDUZI WA ILANI YA UCHAGUZI NA KAMPENI ZA CHADEMA/UKAWA JANGWANI JANA

 

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji wakiwasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

Umati wa wakazi wa Jijini Dar es salaam, ukiwa umefurika kwa wingi kwenye viwanja vya Jangwani kuwalaki Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho,  Agosti 29, 2015.

Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakiwashangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho,  Agosti 29, 2015.

Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakionyesha furaha yao kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015.

Sehemu ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali nchini wakiendelea kuchukua habari za Mkutano huo, uliofanyika jana jioni  kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam na kuhudhulia na maelfu ya Wakazi wa jiji hilo.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akimkabidhi, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, Kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa mwaka 2015/2020 mara baada ya kuizindua.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakionyesha vitabu cha Ilani ya Uchaguzi mara baada ya kuzinduliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe.

Viongozi wa Vyama mbali mbali vinavyounda UKAWA wakionyesha Ilani hiyo mbele ya maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (kulia) akiwatambulisha baadhi ya Wagombea Ubunge katika Majimbo mbali mbali ya jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia akizungumza kwenye Mkutano huo.

Watu wa Msalaba Mwekundu wakiwa wamembeba mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar aliepoteza fahamu kwa kukosa hewa kutokana na uwingi wa watu uliofurika kwenye viwanja vya Jangwani, Jijini Dar es salaam.

Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akitoa salamu zake kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam .

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mgombea Mwenza wake, Mh. Juma Duni Haji, wakati wa Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akihutubia katika Mkutano huo wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho.


Mmoja wa wanasiasa wakongwe waliotoka CCM, Tambwe Hiza akisalimia.








Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO