Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA yawakatia Rufaa Waliotangazwa Kupita Bila Kupingwa

 

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekata rufani katika majimbo matatu ya Bumbuli, Mlalo na Ludewa baada ya pingamizi zake kutupiliwa mbali.

Pingamizi hizo zilitupiliwa mbali na Wasimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo hayo na hivyo kuwatangaza wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamepita bila kupingwa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala, alisema tayari wamewasilisha rufani na wanasubiri uamuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na wanaamini haki itatendeka.

Alisema Jimbo la Ludewa, Msimamizi wa Uchaguzi, alidai kwamba katika fomu ya mgombea wa Chadema haikuwa na fomu namba 10, huku mgombea akisema aliwasilisha kila kitu kinachohitajika ikiwamo fomu hiyo.

Kibatala alisema baada ya kufuatilia, ofisi ya msimamizi ilibaini kwamba wao ndiyo walifanya uzembe katika kuihifadhi. Alisema sababu za kutupiliwa mbali pingamizi katika majimbo mengine, hazikuwa na msingi hususan Majimbo ya Bumbuli, Mlalo, Peramiho, Handeni Mjini na Chalinze na hivyo kulazimika kukata rufani.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu, alisema sababu za wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo hayo kutupa pingamizi hizo, siyo za msingi na inaonekana wamepanga kuwabeba wagombea wa CCM wapite bila kupingwa.

Akizungumza na Nipashe, Mkurugenzi wa Uchaguzi Nec, Ramadhani Kailima, alisema hakuwapo ofisini wakati rufani hizo zinapelekwa, lakini alisema anaamini zitafanyiwa kazi.

“...lakini kama wamesema wameleta, yamepokelewa na yatafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.

Nec ndiye muamuzi wa mwisho katika suala hilo na ikishatoa uamuzi hauwezi kupingwa popote ikiwamo mahakamani labda yawe ni jinai yanayohusisha matusi au rushwa,” alisema.

KUZINDUA KAMPENI JUMAMOSI

Na katika hatua nyingine, Mwalimu alisema Ukawa watazindua kampeni zake Agosti 29, mwaka huu katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia sababu za awali kutaka kuutumia Uwanja wa Taifa katika uzinduzi huo, alisema ni za kiusalama, idadi kubwa ya wafuasi wao.

Hata hivyo, alisema wameshangazwa na serikali kuwanyima uwanja huo kwa kutumia kigezo ya mihemko mikubwa ya kisiasa na kwamba kitendo hicho ni muendelezo wa kuminya demokrasia nchini.

Pingamizi la Mgombea wa CCM dhidi ya Chadema, latupiliwa mbali.

Na Bryceson Mathias, Mvomero-Morogoro.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Sadiq Murad, dhidi ya Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Osward Mlay, wa Jimbo la Mvomero, Morogoro.

Akizungumza na Tanzania Daima, Mchungaji Mlay amekiri kuwekewa Pingamizi na Murad aktilia shaka Jina a Elimu yake, ambapo Mchungaji Mlay amesemaalmelijibu na limetupiliwa Mbali na anaendelea na Maandalizi ya kufungua Kampeni.

“Ni kweli niliwekewa Pingamizi na Mgombea Mwenzangu (Murad) wa CCM, lakini nadhani alikosa Uelewa, lakini nimelijibu Pingamizi lake na limetupiliwa mbali, na sasa najiandaa kwenda Morogoro kwa maandalizi ya Kampeni.

“Naomba niombeani, kimsingi hatuna muda wa kujadiliana na Watu ambao, Mungu amemwinua Musa aende kwa Farao, awatoa Watu waende nchi ya Maziwa na Asali, amemwinua Yusuf, akaandae Chakula kwa Miaka Saba ya Njaa inayokuja, halafu mtu anazuiamia, anazuia! Tusimkubali”.alisema Mlay”.

Chma kimenichagua nipeperushe Bendera ya Chadema, kwa hiyo katika hili, Wananchi na Wanachama wenye Uchungu wa Mateso waliyofanyiwa na CCM kwa Miaka 50 ya Uhuru, ambapo haki za Wafanyakazi, Wafanyabiashara, Wakulima na Wafugaji, zimekuwa zikiporwa, wajipange tuvuke Ng’ambo ya Mto.

Aidha aliwataka Wananchi, Viongozi wa Dini, akina Baba, Wazee, akina Mama na Vijana wa Jimbo la Mvomero, wasiichezee nafasi hii ambayo Mungu amewapa Wana Mvomero, wakabaki kuzunguka kwenye Mlima wa Seiri, ila wageuke upande wa Kulia uliko Ukombozi wa Mungu.

‘Wana Mvomero, Mlivyozunguka Mlima huu (wa adha na dhuluma za CCM kwa Miaka 50 ya Uhuru) Vyatosha, geukeni pande wa Kaskazini.”alisema Mchungaji Mlay, akinukuu Maandiko Matakatifu ya Biblia, Kumbukumbu la Torati Sura ya Pili 2 Mstari wa Tatu(Kumb.2:3)


CHANZO: CHADEMA BLOG

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO