Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

JK kusaini mikataba mitatu ya kiitifaki - Nipashe

 

 

Rais Jakaya Kikwete, amepanga kuhitimisha miaka 10 ya utawala wake, kwa kusaini mikataba mitatu ya kiitifaki ikiwamo malengo 17 ya Ajenda ya Maendeleo Endelevu Duniani (SDG’s), uhitimishaji wa Malengo ya Milenia na Mkataba mpya wa Mabadiliko ya Tabia Nchi ambao utarithi Itifaki ya sasa ya Kyoto.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge, alisema Rais Kikwete na wakuu wengine wa nchi za Afrika, watasaini makubaliano ya wataalam wa pande zote duniani, Septemba, mwaka huu.

Alikuwa akizungumza katika maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa (UN), yaliyofanyika jana katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa), kwa kupanda miti 2,400 kwenye eneo la msitu mnene wa Nusu Maili.

“Utekelezaji wa Mkataba wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu, utaanza mwezi Januari mwaka 2016, ukiwa na dhumuni la kugawana utajiri na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi; wakati Mkataba wa Itifaki ya Kyoto utaanza kutekelezwa na nchi zote duniani mwaka 2020,”alisema Dk. Mahenge.

Hata hivyo, Makamu mwenyekiti wa Taasisi ya Uhifadhi wa Mazingira (TEACA), Adoncane Mcharo, aliiomba serikali kukubali ombi la wakazi wa vijiji 39 vinavyoizunguka Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, kupewa hati maalum ya kumiliki eneo la msitu wa Nusu Maili.

Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez, alisema ujio wa ajenda hiyo mpya ya maendeleo endelevu ambao utatekelezwa kwa miaka 15, baada ya kumalizika kwa Changamoto za Maendeleo ya Milenia, kutaihakikishia dunia kufanikiwa katika vita ya kutokomeza umasikini, njaa, magonjwa na machafuko.

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Celestine Mushi, alisema katika kukabiliana na umasikini, njaa na mabadiliko ya tabia nchi, wataalam kutoka mataifa mbali mbali, Agosti 2, mwaka huu, walikutana nchini Marekani na kuafikiana mikataba hiyo isainiwe na wakuu wa nchi kabla ya kumalizika mwaka 2015.

Awali, Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Novatus Makunga aliueleza ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa na mabalozi kutoka nchi mbali mbali kwamba hatua hiyo ni katika kuzuia mabadiliko ya tabia nchi yasiendelee kuathiri uoto wa asili na volcano ya mlima huo.

CHANZO: NIPASHE

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO