Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TAARIFA ZILIZOENEA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU MKUTANO WA DKT. BILAL SI ZA KWELI

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasikitika kuwepo kwa taarifa za uzushi ambazo zimesambaaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo vya habari kuhusu msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.

Habari hizi si za kweli na tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais, hausiki na taarifa hizo zilizoenea kwenye mitandao ya Kijamii na wala hajapanga tukio lolote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.

Aidha tunatumia nafasi hii kuwataka wale wote wenye tabia ya kuvumisha taarifa zisizo sahihi kwa maslahi yao waache kufanya hivyo kwa kuwa ni kosa kisheria. Tunawaomba waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi na kutafuta taarifa sahihi kwenye vyombo vinavyohusika na kutambulika.


Boniphace Makene

Mwandishi wa Habari wa
Makamu wa Rais

10/8/2015

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO