Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Yafahamu hapa Maswali 6 Aliyoulizwa Dr SLaa na Waandishi wa Habari Baada ya Kutangaza Kuachana na Siasa za Vyama leo


Slaa
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dr Wilbrod Slaa ametangaza kuachana na siasa hii leo. Hatua hii inakuja kwa kile alichodai kutokubaliana na wenzake ndani ya CHADEMA kumpokea Lowassa na kumpa nafasi ya kuwa mgombea wa chama hicho.

Dr Slaa amesema atakuwa mtu binafsi asiye kuwa na chama lakini ataendelea kushiriki kwenye masuala yanayohusu siasa bila kuwa na uanachama wa chama chochote. Hii inathibitisha kuwa yeye sio mwanachama wa CHADEMA tena.

Yafuatayo ni baadhi ya maswali ambayo aliulizwa na waandishi wa habari na kuyajibu baada ya kipindi cha hotuba yake kwa takribani lisaa limoja kumalizika.

1. Umetangaza kustaafu siasa (na kuachana na siasa za vyama) na uka kadi mbili (za CCM na CHADEMA). Je, nazo utazirudisha!?

Majibu: Kadi ni mali yangu. (sitairudisha)... Sijawahi kufanya kazi ya CCM.

2. Umesema waliopokelewa CHADEMA wengine ni makapi. Mwaka 1995 ulihama CCM. Je, nawe ulikuwa kapi!?

Majibu: Mimi sikuwa mbunge niliyekataliwa. Sikuwa mwenzao, sikuwa mla rushwa.. Kama ni kapi pima mwenyewe.

3. Ulituambia kuwa Lowassa angekuwa ni asset (kwa CHADEMA kwa vigezo ulivyoweka wakati wa kumkaribisha, angekuja na wabunge 50, wenyeviti wa CCM mikoa 22 na wenyeviti wa CCM wilaya 80). Je yangetimia hayo huu chafu wa Lowassa ungefutika!?

Majibu: Nilisema nina vigezo viwili (kumkubali Lowassa), kama ni Asset ama Liability. Baada ya kujiridhisha na hayo mnafanya tathmin. Angetimiza hayo..hakufanya yote.. sina la kulalamikiwa.

4. Unaonekana kumshambulia sana Lowassa. Je, hii ni baada ya kukosa nafasi ya kugombea Urais CHADEMA?

Majibu: Nilieleza mwanzo. Slaa hajagombea urais, unakasirikaje kama hujachukua fomu? Sina ugomvi wala chuki na yeyote. Sina ugomvi na Mbowe. Mbowe ni rafiki yangu, hata nyumba ninayoishi alinisaidia. mimi ni masikini.

5. Kwa kutumia mfano wako wa kwamba ukihamisha choo na kukiweka chumbani, harufu ya choo itabaki ile ile.
Wewe uliweza kutoka CCM na kubadili CHADEMA. Je, waliotoka CCM sasa kama wewe hawawezi kuibadili CHADEMA (kufuata kanuni na taratibu)!?

Majibu: Dr SLaa hakuwa mchafu. Tatizo sio kuhama chama. Hakuna tatizo kuhama chama.

6. Unadhani nani anafaa kuwa Rais kwa uchaguzi wa Oktoba 25, 2015!?

Majibu: Nimeeleza tu taifa litakuwa na madhara gani huyu (Lowassa) akiwa Rais. Watanzania waache ushabiki ambao baadae watajuta. Sikuja kumtetea mtu... Kama utetezi wangu utakuwa wa upande fulani, sina namna nyingine ya kueleza.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO