Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Breaking News! Ajali Dodoma..Mtoto Kikwete agongwa na gari na kufariki hapo hapo, wananchi wafunga barabara!

Muda huu Blog hii imepokea taarifa kuwa wananchi wenye hasira wamefunga barabara inayoelekea Singida kutoka Dodoma eneo la Msembeta ambalo liko nje kidogo ya Mji wa Dodoma baada ya mtoto wa darasa la nne, aliyetambuliwa kwa jina la Kikwete Mswaga kugongwa na gari na kufariki hapo hapo jirani kabisa na eneo la kuvukia kwenda shuleni.

Gari iliyomgonga inaelezwa kuwa ni gari kubwa..semi tariler, ambapo tunaendelea kufuatilia namba na jina la dereva sambamba na chanzo cha jali hiyo.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO