Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MUHIMU!!–KUJIANDIKISHA KWA AJILI YA QT NA KURUDIA MITIHANI YA FORM FOUR MWISHO APRILI 30, 2013

clip_image002

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia Watahiniwa wote wa Kujitegemea wanaotarajia kufanya Mtihani wa Maarifa (QT) na Kidato cha Nne (CSEE) Mwezi Novemba 2013 kwamba Usajili utafungwa rasmi tarehe 30/4/2013.

Baraza la Mitihani linasisitiza kuwa hakuna mtahiniwa atakayesajiliwa baada ya tarehe 30/4/2013. Hivyo watahiniwa ambao bado hawajajisajili hadi sasa wanashauriwa kujisajili mapema iwezekanavyo kabla ya usajili kufungwa. Usajili unafanyika kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz.

IMETOLEWA NA:

KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO