Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Mkutano wa Chadema Loliondo Jumamosi hii; Lissu asimulia historia ya mgogoro wa ardhi ya Loliondo

DSC09650Sehamu ya wananichi wa Soitsambu waliojitokeza katika mkutano wa Chadema eno hilo siku ya Jumamosi Aprili 6, 2013. Katika mkutano huo Chadema iliwakilishwa na viongozi wake ambao pia ni wakurugenzi katika chama akiwemo Mh Tundu Lissu, Mh Peter Msigwa.

Lissu alihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika Kijiji cha Soitsambu juzi, alisema kuwanyang’anya ardhi Wamaasai ni muendelezo wa dhuluma inayofanywa na serikali dhidi ya jamii hiyo tangu enzi ya ukoloni ambapo walifukuzwa kutoka eneo la hifadhi ya sasa ya Serengeti mwaka 1958/59.

Alisema baada ya uhuru, serikali iliendelea kutwaa ardhi za Wamaasai kwa kuanzisha hifadhi za taifa za Manyara, Tarangire na Arusha huku maeneo mengine katika wilaya za Simanjiro, Monduli, Kiteto na Longido yakigeuzwa mapori ya akiba.

Lissu alisema kuwa badala ya kufikiria kuwahamisha wafugaji hao, ilipaswa kuwapongeza kwa kumudu kuhifadhi mazingira na wanyamapori katika maeneo yao tofauti na makabila mengine nchini yaliyoharibu mazingira na kuua wanyamapori kwenye maeneo yao.

Naye Mch. Msigwa aliwataka Wamaasai kuonyesha hasira yao kwa kukinyima kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika chaguzi zijazo kuanzia serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu ujao 2015

Viongozi wengine lwaliohudhuria mkutano huo ni James Millya, Katibu wa Kanda ya Kasakazini Bw Amani Golugwa, Katibu wa Wilaya Arusha Mjini, Bw Sarungi, Mwenyekiti wa Vijana Mkoa Mh Ephata Nanyaro, Mwenyekiti Vijana Wilaya Bw Noel Olevaroya.

Viongozi na watu wengine walioambatana na msafara huo ni Kiongozi wa Vijana Wilayani Hai, Bi Doris Cornel, Christopher Mbajo toka Same, Katibu wa Vijana Wilaya Arusha Mjini, Glory Kaaya, Kamanda Magoma Jr Magoma na Kiongozi wa Vijana Kata ya Sekei, Ndg Bahati.

DSC09660

DSC09653Katibu wa Vijana Wilaya ya Arusha (CHADEMA), Bi Glory Kaaya katika pozi na wanawake wa Ngorongoro

DSC09655Kina mama wakionesha ishara ya vidole viwili inayotumiwa na Chadema, mwenye rubega nyekundu ni mwanaChadema toka Arusha, Doris Cornel

DSC09664Benchi la viongozi wa Chadema

DSC09658Katibu Mkuu wa Chadema Mkoa wa Arusha ambae pia ndie Katibu Mkuu wa muda Chadema Kanda ya Kasakazini, Mh AMani Golugwa (mwenye suti nyeusi) akishauriana jambo nakiongozi mwenzake

DSC09649Christopher Mbajo (mwenye miwani) mdau mkubwa wa Blog hii alikuwepo

DSC09657

DSC09672Mwananchi akitoa ushuhuda

DSC09662Wana Soitsambu wakifuatilia hotuba za viongozi wa Chadema juzi

DSC09666Baadhi ya viongozi wa Chadema Mkoa wa Arusha, pamoja na James Millya

DSC09671Magaoma Jr Magoma akiangalia kitu kwenye iPad yake huku baadhi ya wananchi wa Soitsambu wakishuhudia. Picha zote na Glory Kaaya

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO