Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Tume ya Uchaguzi yaibua utata Arusha

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeibua mtafaruku mkubwa wa kisiasa mjini Arusha, baada ya kutangaza kata nne kufanya uchaguzi mdogo na kuiacha Kata ya Sombetini ambayo aliyekuwa diwani wake, Alphonce Mawazo (CCM) alihamia CHADEMA.

Ratiba hiyo iliyotangazwa juzi na Mkurugenzi wa NEC, Julius Mallaba inaonesha kuwa uchaguzi huo mdogo utafanyika katika kata 26 kwenye halmashauri 21 zikiwemo nne za Arusha Mjini za Kimandolu, Elerai, Kaloleni na Themi.

Madiwani wa kata hizo nne walivuliwa uanachama na chama chao cha CHADEMA baada ya kukiuka taratibu na katiba huku Kata ya Sombetini ikiwa wazi baada ya Mawazo (pichani) kujiondoa CCM.

Hata hivyo, taarifa ya NEC kutoiingiza Kata ya Sombetini katika ratiba ya uchaguzi mdogo, imeibua hisia mbaya za kisiasa huku CHADEMA wakidai ni mkakati wa kuilinda CCM ili isiipoteze kata hiyo.

Kumekuwa na madai kuwa Mawazo hakuwahi kuandika barua ya kuitaarifu NEC kuwa alijiuzulu udiwani na kuhama CHADEMA, jambo ambalo alilikanusha.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa simu, Mawazo alisema amesikitika kuona tume hiyo haitangazi uchaguzi katika kata hiyo wakati alishahama CCM kwa kuandika barua kwa viongozi wa Manispaa ya Arusha.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema wao wanafuata utaratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Hata hivyo alisema kuwa watawasiliana na Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia ili aweze kulitolea ufafanuzi suala hilo.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema aliliambia gazeti hili jana kuwa NEC inafanya kazi kwa maelekezo ya CCM, jambo ambalo linaashiria kuwa hakuna utawala bora nchini.

“Tume inashirikiana na CCM kupanga ni uchaguzi upi ufanyike lini na upi usifanyike kwa maslahi ya kuilinda CCM, na mimi kama mbunge ninahitaji uwakilishi wananchi wa Sombetini, tume isifanye siasa,” alisema.

Kata zingine na halmashauri zake kwenye mabano ni Stesheni (Nachingwea), Nyampu Lukano na Lugata (Sengerema), Genge Tingeni (Muheza), Ibugule (Bahi), Langiro (Mbinga) na Manchila (Serengeti).

Nyingine ni Iyela (Mbeya), Mbalamaziwa (Mufindi), Ruzewe Mashariki (Bukombe), Mianzini (Temeke), Dalai (Kondoa), Minepa (Ulanga), Makuyuni (Monduli), Bashnet (Babati), Iseke (Singida), Dongobesh (Mbulu), Ng’ang’ang’e (Kilolo), Ifakara (Kilombero), Msanze (Kilosa) na Mnima (Mtwara).

Mbali na uchaguzi huo wa madiwani, pia tarehe hiyo, Juni 16 mwaka huu, NEC imetangaza uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Chambani-Pemba kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wake, Salum Hemed Hamisi aliyefariki Machi 28, mwaka huu.

Chanzo
Stori: Tanzania Daima
Picha: Arusha Times

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO