Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WASIFU WA MAREHEMU FATUMA BINTI BARAKA A.K.A BI KIDUDE.

Marehemu Bi Kidude alikuwa ni gwiji wa muziki katika Bara la Afrika.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Bi Fatma Baraka Khamis,(Kidude) baada ya kutunukiwa nishani ya Sanaa na Michezo na Rais wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,(kulia) katika sherehe za kutunuku Nishani katika Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam. Picha na
Ramadhan Othman, Ikulu.

Tamalyn with 100 year old songstress, dancer and healer, Bi Kidude

Jina lake halisi ni Fatuma binti Baraka. Bi Kidude ni msanii mkongwe na mahiri sana katika fani ya muziki wa mwambao ambao hujulikana kwa jina la Taarabu.

Muziki huu ambao ni mchanganyiko wa muziki toka nchi za Kiarabu na vionjo vya muziki wa Kiafrikaumekita sana katika mwambao wa Afrika Mashariki yaani Zanzibar, Mombasa, Lamu na kwingineko.Leo hii ni Marehemu !.

Nguli na Mtunukiwa wa Nishani ya Uhuru wa Tanganyika/Tanzania 2012, Fatuma binti Baraka au Bi Kidude, alizaliwa katika kijiji cha Mfagimarigo Zanzibar katika familia ya watoto saba (7). 

Baba yake Mzee Baraka alikuwa ni mfanyabiashara wa nazi, zao ambalo ni la kutumainiwa sana Zanzibar.

Bi Kidude aliwahi kusimulia kuwa hafahamu tarehe halisi aliyozaliwa, isipokuwa anachojua ni kwamba alizaliwa wakati rupia ikitumika kama fedha, na vilevile ana hakika ni kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Ulaya.
Wataalamu wa mahesabu baada ya kupata taarifa hizo wakampigia mahesabu na kumkabidhi miaka yake kwamba ni zaidi ya miaka 90.

Bi Kidude aliendelea kusema uimbaji aliuanza tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi na alijifunza kutoka kwa msanii mkongwe na aliyetamba sana enzi hizo Sitti binti Saad.

Anasema wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakifika Zanzibar kuja kumwona Sitti, na kwa vile Bi Kidude na Sitti walikuwa wako karibu basi yeye alikuwa akiwapeleka wageni wale nyumbani kwa Bi Sitti, wakifika huko wageni walikuwa wakiingia ndani na yeye kubakia nje, kule ndani Bi Sitti alikuwa akiwaimbia wale wageni, na yeye huku nje alikuwa akimsikiliza kwa makini na kumfuatiza jinsi alivyokuwa akiimba. 

Aliendelea hivyo hadi akawa mahiri sana katika uimbaji.Alipokuwa na miaka 13, kwa mara ya kwanza alitoroka nyumbani kwao Zanzibar na kukimbilia Tanzania Bara, baada ya kulazimishwa kuolewa. 

Lakini alipokuwa kigoli wa kutosha kuolewa aliolewa ingawa ndoa hiyo nayo haikudumu kutokana na manyanyaso aliyokuwa akiyapata, hivyo aliamua kukimbilia kaskazini mwa Misri ikiwa ni katika miaka ya 1930, huko aling’ara sana katika fani yake ya uimbaji na uchezaji ngoma. 

Lakini ilipofika miaka ya 1940 aliamua kurudi nyumbani Zanzibar ambako aliendelea na shughuli zake uimbaji.

Bi Kidude hategemei kazi moja tu ya kuimba, kwani pia ni mfanyabiashara ya ‘wanja’ na ‘hina’ ambavyo anavitengeneza yeye mwenyewe, pia ni mtaalamu wa matibabu kwa dawa za mitishamba na zaidi ya hayo ni mwalimu mzuri sana wa ‘Unyago’ na ameanzisha chuo chake mwenyewe na anasema katika wanafunzi wake wote hakuna aliyepata talaka kutoka kwa mumewe.


Watu wanasema ‘Utu uzima dawa’ Bi Kidude ana upeo mkubwa sana wa akili kwani pamoja na kukulia katika mazingira yaliyogubikwa na tamaduni za kiarabu ambapo mwanamke anatakiwa wakati wote akiwa hadharani ajifunike, Bi Kidude aliliona hili katika upeo mwingine kwamba ni sheria tu ya kitamaduni toka Uarabuni, hivyo aliamua kuvunja sheria hiyo na kuondoa hijabu mwilini mwake, na sasa hivi anavaa kama Mtanzania na si kama Mwarabu. 

Lakini hakubakia hapo alivunja na miiko mingine zaidi ya kutokunywa na kuvuta, kwani Bi Kidude anakunywa pombe na kuvuta sigara jambo ambalo si kawaida kwa wanawake Zanzibar.

Bi Kidude amekwisha tembelea nchi nyingi sana ikiwa ni pamoja na Oman, Ufaransa, Hispania, Ufini, Ujerumani na Uingereza.

Amekwisha pata tuzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) mwaka 1999 tuzo ni ya maisha. Pia mwaka jana tuzo ya WOMAX ilienda kwake.

Nyimbo alizowahi kuimba ni pamoja na Muhogo wa Jang’ombe, na anaimba kwa Kiswahili na Kiarabu. 

Hakuwahi kupata elimu nyingine zaidi ya Kurani.

Bi Kidude pia amekuwa akishirikishwa na wasanii wengi wakongwe na chipukizi katika nyimbo zao. 

Miongoni mwa nyimbo zinazotamba sana siku hizi ambazo Bi Kifude ameimba na vijana wa kisasa ni za Msanii Ali Toll maarufu AT.

Mbali na AT lakini pia Bi Kidude amewika na kung’ara zaidi katika wimbo mwingine wa vijana wa Ahmada Umelewa wa Msanii Offside Trick ambao umepigwa marufuku kupigwa kwa sasa visiwani Zanzibar.

MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI FATMA BINTI BARAKA AMINA

**TAARIFA KWA HISANI YA JUMA MTANDA**

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO