Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Maoni ya Baadhi ya Wananchi Kuhusiana na Mwenendo Mzima wa Vikao Vya Bunge Hususani Lugha Chafu Toka Kwa Wabunge na Uimara wa Usimamizi wa Bunge Baada ya Wabunge 5 Kutolewa nje Kikao Cha Jana.

MAONI HAYA NI KWA MUJIBU WA TOVUTI YA GAZETI LA MWANANCHI TAR 18 APRILI 2012 AMBAPO WANANCHI MBALI MBALI WAMEWEZA KUTOA MAONI YAO KUFUATANA NA HABARI ILIYOPO KWENYE TOVUTI HIYO IKIHUSU VURUGU ZILIZOIBUKA BUNGENI JANA, HABARI AMBAYO UNAWEZA KUISOMA PIA KWA KUBOFYA HAPA

Photo

Taswira ya vurugu zilizotokea Bungeni Dodoma jana ambapo Mbunge wa Mbeya Mh Mbilinyi akiskiwa pamoja na Wenje, Lema na wengineo wakionekana kwa pamoja wakiwazuaia askari ili wasimtoe nje Mh Tundu lissu aliyeamriwa na Naibu Spika, Job Ndugai atolewe nje ya ukumbi wa Bunge kwa kuadiwa kuomba muongozo sana.

Naibu Spika Ndugai jana  aliamuru Tundu Lissu atolewe nje ya Bunge huku wabunge wa upinzani wakizomea na kuseama hatoki mtu.

Amri hiyo ilitokaea baada ya yeye  kuingilia kati mchango wa Mwigulu Nchemba aliyesema kwamba udini ni jambo geni hapa nchini na kwamba Tanzania imeongozwa na CCM tangu uhuru, na marais wote wamekuwa wakitoka ccm, rais wa kwanza alikuwa mkristo, wa pili muislam, wa tatu mkristo na wa nne ni muislam..akasema kama udini ni jambo geni watanzania tujiulize limekujaje???? Kwanini sasa na sio wakati huo? Picha na mitandao ya kijamii

********************************

Evordy Millinga

Nafikiria sasa wakati umefika wa kujua pumba ni zipi na mchele ni upi? Hii inatia aibu" tena inafedhehesha kabisa kwa Bunge kama hili linavyoendeshwa tena na aina ya wabunge tulio nao!? Yaani ni Bora posho kuliko kusikiliza na kwasilisha maisha ya watanzania"
Hivi wabunge wa upinzani wakiongea au kukosea ni makosa?kwanini wabunge wa CCM mnakuwa siwaungwana au kwasababu mnatawala Dola?acheni unafiki hebu wasikilizeni wenzenu,hata mtu akisimama mara elfu hiyo siyo sababu ya kuwafanya Kiti" atoe maamuzi yasiyo faa yaani ubabe" Hawa kina Mwigulu ni watu wanaotaka kuharibu Bunge kwakujiona wanajua kwa kusema uongo" Tafathalini CCM mwangalieni mtu huyu hawafai Mbona Kina Mzee Leizer wana Hekima?Filikunjombe ni makini sasa hao akina Stela manyanya,serukamba ,Rage nk.....Mnamatatizo gani? au Mmetumwa mtuharibie Nchi?mpo kwaajili ya nani?Chonde chonde hapo siyo kijiwe cha mipasho na matusi......Tuwe makini jamani!

************

(Huyu hakujitambulisha)

Bunge hovyo, spika na naibu spika wameshindwa kuliongoza bunge. Kuna upendeleo wa wazi kabisa, ambao hata mtoto wa miaka mitano anaweza kuuona, wakitukana wabunge wa CCM ni sawa, wala hakuna adhabu. Huyu Serukamba ametukana bungeni "fuck you" hajapewa adhabu yeyote, au naibu spika hakumsikia????. Lusinde ameporomosha matusi na kudhalilisha kina mama, hakupewa angalau karipio. Mbunge wa Chadema akisema ukweli , anaambiwa ametowa lugha ya kuudhi au amemdhihaki rais. Na mara moja anapewa adhabu ya kutolewa nje, au anaamriwa kudhibitisha. Tunakwenda wapi?
Hii ni double standard. Spika na naibu wako mjiuzulu, majukumu mliyopewa ni makubwa kuliko uwezo wenu.

**************

Wabunge wajibu wao ni kusimamia serikali uliyopo madarakani sasa nashangaa sana kuona wabunge wa CCM jinsi watendayo...NDIVYO WAFANYANVO UPINZANI KUKOSOA SERIKARI KWA VIELELEZO SAHIHI, ILI SERIKALI IBADILIKE lakini wao CCM yaani wapo kishabiki shabiki tu. Kama Injini mzima Stella anasimama kuwarushia maneno wabunge wapinzani badala ya kuchangi hoja za msingi kwa maaendeleo ya Watanzania,...Hakika ifike wakati hata Spika na mawaziri wasiwe na uhusiano na siasa (wanasasiasa). PIA KUWEPO NA UTARABITU WA KUJADILI UFUMBUZI WA MATATIZO YA WATANZANIA NA UTENDAJI/UPUNGUFU WA SERIKALI NA SI KUJADILI CHAMA AU MWANACHAMA kama wafanyavyo hao majority bungeni

******

Kasuku1

Namuomba mweshimiwa raisi kama mweketi wa chama na najua yeye na viongozi wenzie ndio waliotuchagulia spika kwa kuingiza kipengele cha kwamba sasa ni zamu ya wanawake katika kupitisha jina la mgombea wa spika kupitia CCM huku wakijua wazi kuwa CCM kwa kuwa ndiyo iliyokuwa na wabunge wengi basi Makinda amabye ndiye aliyekuwa mteule wao lazima angepita. Sasa namuomba ikiwezekana atuondolee makinda na kuturudishia Sita wetu kwani enzi zake aliongoza bunge kwa umakini mkubwa na kila mtu alipenda kusikiliza bunge na bunge lilikuwa na hadhi kubwa mbele ya jamii lakini sasa limepoteza mwelekeo chini ya huyu mama ambaye nadiriki kusema ameshindwa kwa kila namna au kabisa kuongoza bunge

****************

rashid.aljabry2008@gmail.com

nina wasiwasi na ndugai kama ana elimu na uelewa wa kutosha na kazi ya naibu spika.Hivi kama serukamba alitukana kwanini aliachiwa kuendelea kuzungumza

****************************

Abdu Hussain Salim

Nchi ina wenyewe na wenyewe ndo sisi upinzani hauna nguvu bungeni semeni sisi tuta pitisha tulitakalo

**********

Asra Daiy

Kiti cha spika kinayumba ndio maana bunge haliwezi kuwa shwari,hali hii haikuwepo wakati wa mzee wa spidi ana viwango mhe.Samweli sita.Jana tumeona jinsi naibu spika alivyokuwa na upendeleo wa wazi,Peter Serukamba mbunge wa kigoma mjini alitukana na sote tumemsikia lakini naibu spika hakufuata maagizo ya spika,kwa kumtoa serukamba nje,lisu alikuwa anataka kutoa taarifa amemtoa nje ,hivi viongozi wa aina hii wanatufaa!.
Wako bungeni kwa ajili ya kuwakilisha wanachi katika kupitisha bajeti ya serikali,kwa kuchangia,kutoa maoni na kuikumbusha serikali kuhusu miradi mbalimbali ya maendelo kwenye majimbo yao ambayo imepangwa kufanyika au hajafanyika pia kuishauri serikali.Nadhani inabidi tuwabane wabunge wetu pindi wanaporudi majimboni huko dodoma wamefanya nini?,au walikwenda kutuonyesha ufahari wa kujua jinsi ya kutukana na huenda wengine wamejifunza hizo lugha chafu,imagine kama baba yako ni yule mhe. wa mtera unajisikiaje?.

**********

Kipara Juakali

Hoja ya serikali kushindwa kutatua migogoro hasa ile ya kidini ni kweli kuwa wameshindwa lakini lakini si kwa ugumu wa tatizo bali kwa MAKUSUDI na kibaya zaidi wanachofanya ni kukamata na kuwafunga watu bila hatia hili ni tatizo kubwaaa.

Maslahi ya chama chao yanapewa kipaumbele kuliko yale ya taifa, wako tayari kuwafunga na hata kuwaua watu wasio na hatia ili washinde uchaguzi 2014/2015 hii ndio dira na farsafa ya watanwala wa tanzania chini ya chama cha mapinduzi.

Lakini chadema nao wanalazimika kujifunza na kubadilisha mwelekeo. Kwa sasa kinaonekana kuwa chama cha commedy zaidi kuliko ilivyotarajiwa na wapiga kura. Hakuna njia ya mkato kuiondoa CCM ispokuwa kuunganisha nguvu na kujenga hija zenye tija badala ya matusi na vurugu mechi kama ilivyo sasa katika Bunge.

Chama cha CUF kilipooongoza kambi ya upinzani bungeni kiljenga hoja na watanzania wakafaidika. Kodi ya kichwa iliondolewa, mikutano ya hadhara ya kisiasa iliruhusiwa bila kibali cha polisi, shule za kata zimejengwa na serikali ya umoja wa kitaifa imepatikana zanzibar. TIJIFUNZE NDUGU ZANGU

***********

Tito Simwita

Imefikia hatua Bunge limekuwa kama sehemu ya Wahuni,jamani hiyo ni sehemu Tukufu ambayo Watanzania wote wanaitegemea kupata haki na maslahi leo inageuzwa kama genge la wahuni.Jamani Wabunge wetu embu kumbukeni viapo venu.

*********

Mick

Wananchi mnatuacha katika masikitiko makubwa sana, kwani tunawasiwasi kama kweli wabunge wetu wanafahamu walichokwenda kukifanya huko bungeni. Mnaleta siasa za vyama na kuendelea kufanya bunge liwe kama klabu ya pombe za kienyeji, bunge hilo ni kwa ajili ya makadirio na matumizi kwa ajili ya maendeleo ya nchi na sio kwa ajili ya kutekeleza matakwa ya kisiasa ya vyama. Wabunge tumieni busara, mmechaguliwa na wananchi wakiwa na matumaini ya kuwakilisha masuala yanayowakera, baadhi yenu mambo mnayoyafanya ni ya aibu, midomo yenu itumieni kuzungumza kama kweli utakacho zungumza utaona kitakuwa na manufaa/muhimu kwa wawakilishi wako/taifa, msifanye kama hilo ni bunge la walevi wabunge wanaropoka tu''. Tunajiuliza watanzani tutegemee kitu gani kwa wabunge wa aina yenu, mtakuwa na uwezo kweli wa kupitia vipengere mbali mbali vya bujeti na kutolea maamuzi yenye mantiki yatakayotupeleka mbele kmaendeleo? aibu, aibu,aibuuuu.

*********

Daniel_Mutani

Inahitaji hekima ya pekee katika kuongoza, shida kubwa wengi wa viongozi wetu wanaongozwa na makundi nyuma yao hivyo ni vigumu kufanya maamuzi sahihi ambayo yangeweza kuwapatia heshima. Kauli za wabunge zinaonesha jinsi walivyo chokana na kwa matendo yao wanachochea na kupaandikiza vurugu na chuki bila wao kujua. Bunge bado nahisi linamwitaji mtu kama Sita (na madhaifu yake kama binadamu) katika kuongoza,, na wengine wengi imara. Haikubaliki kuona aibu tunayoiona sasa ingawa kweli kuna mabadiliko katika jamii (social change). Nafikiri tunahitaji viongozi wasio na upendeleo wenye uwezo wa kukemea. Kama Serukamba alikosea na wale wabunge walionekana kukosea, basi wote wangetolewa ama kuchukuliwa hatua..inashangaza kuona aliyetukana hata gazeti hili limeshindwa kuandika aina ya tusi ameachwa na wenye maneno yalioorodheshwa humu wamechukuliwa hatua.. Tutafakari wapi tumekosea na tusawazishe

*********

Noah

Chadema hata km wanajua ukweli wa kitu, hawakubali kushindwa, hilo tu ndilo linanichukiza, mtu anajua kabisa kanuni inasema hivi lkn atang`ang`aniazia kitu alimradi haonekane yuko sawa.

********

Zakayo Mwalongo 

CCM waache ubabe, Serukamba alitukana tusi ambalo hmna anayeweza kuliandika hapa walimfanya nini, lakini wabunge wa CHADEMA wakikosoa kikatiba wanafukuzwa. Spika na naibu wake hawawezi kazi

*********

Dan Mtweve

Mimi nataka kujua tu, je kuna ukomo wa kutoa taarifa maana kama mbunge mmoja anatoa madai ambayo upande mwingine kuwa sio sahihi Ndugai anataka kambi ya upinzani wanyamaze tu!
Ndugai umeonyesha udhaifu mkubwa sana upendeleo wa waziwazI hilo hata kipofu haulizi kuwa wewe unampendelea nani!

***********

KATATANAMA

Spika naye aache kuropoka ili kufurahisha nafsi yake. Juzi alisema yeyote atakaye tukana atachukuliwa hatua. Sasa mbona hatua hazijachukuliwa kwa huyo mbunge aliyeoza mdomo? Au zipo kwa ajili ya upinzani tu?

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO