Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HALMASHAURI YA MERU YATUMIA MIL 30 KUNUSURU WAANGA WA MAFURIKO

DSCF8888

DSCF8897

DSCF8886
Bibi Mwajuma Hassa(80) akiwa na mwanaye Sesilia Hassani(60)wakichambua mboga aina ya mlenda ambapo wamedai kuwa njaa imekuwa tishio kijijini hapo huku akisisitiza kuwa wakati mwingine inawabidi kula mlenda na maji kama chakula

DSCF8890

DSCF8886DSCF8902

Mbunge Nassari akiwa na mkea wa Mazengo aliyevunjika miguu mara baada ya kutembelea nyumba yake ambapo alitoa ahadi ya kumjengea nyumba

DSCF8898

Mico Mazengo ambaye pia ni mwanzilishi wa chama cha ccm(81) akielezea namna nyumba yake ilivyodondoka na kumuangukia mke wake hadi kuvunjika mguu

DSCF8901

DSCF8872

DSCF8869

DSCF8868

DSCF8867

Aliyevalia kitenge ni Makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Frida Kaayapamoja na madiwani

DSCF8865

DSCF8864

DSCF8878

Mh.Joshua Nassari akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo uliowezeshwa na halmashauri hiyo akiwa kati ya   madiwani wa halmashauri ya Meru.

DSCF8879

“Tunapakua unga wa msaada“

DSCF8877

Moja ya nyumba iliyoharibika vibaya  kutokana na mvua kubwa iliyoshesha na kusabaisha mafuriko

DSCF8876

DSCF8875

DSCF8874

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Mh.Jopshua Nassary akijadili jambo na madiwani wa halmashauri ya Meru

DSCF8884

Mazingira halisi ya nyumba ya Bibi Mwajuma Hassani katika picha

DSCF8883

DSCF8882

Bibi wa miaka (80 Mwajuma Hassani amabye ni mkazi wa kata ya Makiba akieleza namna mafuriko yalivyo athiri makazi pamoja na mashamba

HALMASHAURI  ya Meru,wilayani Arumeru mkoani Arusha, imetoa msaada wa unga na maharage na mchele  kwa kaya 1200 zilizokumbwa na mafuriko katika kata tatu za halmashauri hiyo, ili kuzinusuru na baa la njaa baada ya wananchi wake kuanza kushindia mboga za majani na maji.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuigawa misaada hiyo, Makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Frida Kaaya alizitaja kata zilizoathiriwa na mafuriko hayo  kuwa ni Makiba ,Mbunguni na King’ori ambapo, halmashauri hiyo kupitia kitengo
cha maafa ilitenga kiasi cha sh,milioni 30mapato ya ndani  kwa ajili ya kuzinusuru
kata hizo.

Alieleza kuwa, wananchi hao waliathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na mvua kubwa zilizofululiza kunyesha wilayani humo na kupelekea maji kujaa majumbani kwa wakazi hao ambapo  vyakula  vya akibavilielea juu ya maji ,huku mazao waliooteshwa yakisombwa na mafuriko.

Aidha alisema baada ya kupata taarifa juu ya mafuriko hayo,kutoka kwa madiwani wa kata husika kamati ya maafa ilitembelea na kujionea uharibifu uliojitokea na kulazimika kutafuta kiasi hicho cha fedha ikiwemo kuomba msaada kwa wadau wa halmashauri hiyo na mabenki mbalimbali yaliliyopo mkoani hapa.

Alisema fedha hizo zilitoshea kununua magunia 125 ya Unga wa mahindi pamoja na magunia 30 ya maharage ambapo yaligawanywa kupitia ofisi za watendaji na wenyeviti wa vijiji wakiwemo madiwani wa kata husika.

Wakipokea msaada huo mmoja wa madiwani hao kutoka kata ya King’ori ,Akundael Nanyaro ,aliipongeza halmashauri hiyo kwa msaada walioutoa kwani itasaidia kunusuru familia zinazokabiliwa na njaa ambazo zinaendelea kuteseka hadi sasa hivi.

Alisema kata hiyo imeathirika sana kwani baadhi ya nyumba
zilizobomolewa na mvua hizo,vyoo kufurika na kutoa vinyesi,mifugo kusombwa na maji pamoja na vyakula kuharibika vibaya hali inayohatarisha afya za wakazi hao.

Naye Afrisa mtendaji wa kata ya Mbunguni,Godfrey Mollel alivitaja
vijiji vilivyokumbwa na athari hiyo kuwa ni Mbunguni,Msitu wa
mbogo,Migungani,Kikuletwa na Shambarai Burka.

Alisema wananchi wa vijiji hivyo hawana chakula kwani wanaishi kwa kubangaiza na mara nyingi wanashindia mlo mmoja wa mboga za majani aina ya Mlenda na maji tu.

Alisisitiza kuwa kata hizo zipo kwenye hali mbaya na kuitaka serikali na wadai wengine kujitokeza kusaidia zaidi kwani msaada walioupata utasaidia kwa muda mchache na baadae wataendelea na hali ngumu ya maisha katika maeneo hayo kwani hawana msaada zaidi ktoka sehemu yeyote.

‘’tunaomba pia tusaidiwe mbegu za mahindi ,mtama na maharage ili
wananchi wapate kupanda upywa kwenye mashamba yao ambayo mazao waliokuwa wamoteza yamesombwa na mafuriko’’alisema Mollel.

CHANZO: PAMELA MOLLEL

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO