Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Sherehe za kuapishwa Uhuru Kenyata kuwa rais mpya wa Kenya zinaendelea….

 

Uhuru Kenyatta hii leo anaapishwa kama rais wa nne wa Jamuhuri ya Kenya kufuatia ushindi wake dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga katika uchaguzi uliofanyika Machi nne.

Ushindi wake wa kwanza katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo, ulihalalishwa na mahakama ya juu zaidi nchini Kenya.

 

Kenyatta na naibu wake William Ruto, wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya uhalifu wa kivita iliyotokana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu miaka mitano iliyopita.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir, anayekabiliwa na kibali cha kukamatwa na mahakama ya ICC, hatakuwepo kushiriki sherehe hizo.

Bwana Kenyatta ni mwanawe rais mwanzilishi wa Kenya, Jomo Kenyatta, na ni mrithi wa mali nyingi sana nchini humo.

Kenyatta aliwahi kuhudumu kama naibu waziri mkuu , waziri fedha, na waziri wa serikali za mitaa chini ya utawala wa rais anayeondoka mamlakani Mwai Kibaki.

Kenyatta mwenye urmi wa miaka 51, ni rais wa kwanza mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuongoza nchi hiyo.

Raila Odinga alipinga vikali ushindi wa Kenyatta na hata kuwasilisha kesi katika mahakama ya juu zaidi.

Baada ya uamuzi wa mahakama uliosema kuwa alichaguliwa kihalali, Kenyatta alisema kuwa serikali yake itashirikiana na na wakenya kuhakikisha kuwa wanawahudumia wakenya wote bila mapendeleo.

Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza chini ya katiba mpya na wa kwanza katika kipindi cha miaka mitano tangu ghasia zilizoshuhudiwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Bwana Kenyatta anatarajiwa kufika mbele ya mahakama ya ICC kwa kesi anayokabiliwa nayo, ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Amekanusha madai hayo.

Kenya imetia saini mkataba wa Roma unaoishurutisha kutii mahakama ya ICC mnamo mwaka 2002.

Lakini nchi nyingi za Afrika zimekataa kuitii mahakama hiyo na hata kutekeleza kibali cha kumkamata rais Bashir anayetakikana na mahakama ya ICC.

Chanzo: BBC Swahili

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO