Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

VIWANGO VIPYA VYA NAULI USAFIRI WA DALA DALA NA MABASI YAENDAYO MIKOANI TOKA SUMATRA

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini na usafiri wa kwenda mikoani. Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo. Viwango vipya vya nauli vitaanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013.

SUMATRA ina wajibu kisheria kuhakikisha pamoja na mambo mengine kuwa maslahi ya watumiaji na watoa huduma za usafiri yanalindwa ili kuwepo na huduma endelevu ya usafiri ulio bora, salama na wenye kukidhi mahitaji.  Aidha SUMATRA ina jukumu la kujenga na kulinda mazingira mazuri na ya kuvutia kwa watoa huduma ili huduma ya usafiri inayotolewa inakuwa katika kiwango na gharama zinazoendana na huduma zenyewe. 

Katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012, SUMATRA ilipokea maombi rasmi kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wa barabara yakiwemo makampuni ya usafirishaji abiria ya Cordial Transport Services P.L.C, Happy Nation Co. Ltd, ABC Trans na Mwesigwa Mtazaha Kazaula yakipendekeza mapitio ya viwango vya nauli za mabasi yanayotoa huduma za usafiri mijini (Daladala) na mabasi yanayotoa huduma katika Mikoa kufuatia ongezeko la gharama za uendeshaji kwa mujibu wa mawasilisho yao.

Wakati maombi ya wamiliki wa Daladala yalilenga katika kuongeza viwango vya nauli kwa 149% ya viwango vya sasa, wamiliki wa mabasi ya masafa marefu waliomba nyongeza kati ya 35% na 48.5%.

Kwa mujibu wa Kifungu Na 18 cha Sheria ya SUMATRA, 2001, SUMATRA iliwashirikisha wadau mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao kuhusu maombi ya wamiliki ya kuongeza viwango vya nauli kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho.

Aidha Mamlaka iliridhia viwango vipya kwa mujibu wa kifungu cha 16  Cha Sheria ya SUMATRA ambacho kinaipa Mamlaka kufanya mapitio ya nauli mara kwa mara kwa kuzingatia gharama za kutoa huduma, maslahi ya watoa huduma, faida, maslahi ya watumia huduma ya kulipa nauli yenye uwiano na gharama za huduma inayotolewa.

Kwa kuzingatia hoja za waombaji, maoni ya wadau, uchambuzi wa menejimenti, haja ya kupunguza gharama zisizo za lazima za uendeshaji na udhibiti wa vitendo vya uvunjaji wa Sheria na taratibu za uendeshaji shughuli za usafirishaji, Mamlaka ya SUMATRA iliamua kuongeza viwango vya juu vya nauli za Daladala kwa wastani wa 24.46%.

Aidha kwa mabasi ya masafa marefu, viwango vimeongezwa kwa 20.3% kwa mabasi ya kawaida,   16.9% kwa mabasi ya daraja la kati na 13.2% kwa mabasi ya daraja la juu.
Mchanganuo wa viwango vipya vya nauli ni kama ifuatavyo:

1. Nauli za Daladala – Jiji la Dar es Salaam


Umbali wa Njia
Kiwango Kipya cha Nauli
Mfano wa Njia
Kilomita kati ya 0 – 10 (Na mipaka ya Jiji Kati)
Sh 400/=
Ubungo – Kivukoni
Kilomita kati ya 11 – 15
Sh 450/=
Mwenge – Temeke
Kilomita kati ya 16 – 20
Sh 500/=
Tabata Chang’ombe – Kivukoni
Kilomita kati ya 21 – 25
Sh 600/=
Pugu Kajiungeni – Kariakoo
Kilomita kati ya 26 – 30
Sh 750/=
Kibamba – Kariakoo

Mamlaka imeandaa majedwali kwa njia zote za Dar es Salaam. Majedwali hayo yanaweza kupatika katika tovuti yetu www.sumatra.or.tz

Nauli ya Mwanafunzi itakuwa Sh 200/= ambayo ni nusu ya nauli ya mtu mzima ya kiwango cha chini cha nauli ya Sh 400/=. Nauli hii itatumika kwa njia zote za Jiji la Dar es Salaam.

2. Nauli za Mabasi ya Masafa Marefu

Daraja la Basi
Nauli ya zamani kwa km-abiria
Nauli mpya kwa km-abiria
Mfano wa kiwango kipya cha nauli kwa baadhi ya njia

Basi la Kawaida kwa njia ya lami
Sh 30.67
Sh 36.89
DSM–Mbeya Km 833
Sh 30,700
Basi la Kawaida kwa njia ya vumbi
Sh 37.72
Sh 46.11
S/wanga-KigomaKm 551
Sh 25,400
Basi la hadhi ya kati (Semi Luxury
Sh 45.53
Sh 53.22
DSM–Mwanza Km 1,154
Sh 61,400
Basi la hadhi ya juu (Luxury)





li kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya nauli na ubora wa huduma ya usafiri, Mamlaka imetoa maagizo kwa wamiliki wa mabasi ya masafa marefu kuboresha maeneo yanayohusiana na huduma ya usafiri kama ifuatavyo:
  1. Wamiliki wa mabasi kutokutumia wapiga debe katika kuuza tiketi za safari
  2. Wamiliki wa mabasi kuhakikisha wanafuata Kanuni za SUMATRA za Udhibiti wa Tozo na Nauli (SUMATRA Tarrif Regulations) ambazo zinahimiiza kuwepo kwa kumbukumbu sahihi za mahesabu ili kurahisisha mapitio ya viwango vya nauli
  3. Kufuata Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni ya usafirishaji abiria
  4. Kutoza nauli kwa mujibu wa daraja la basi lenye sifa kamili la daraja husika kama ilivyoainishwa katika Kanuni za Usalama na Ubora
Aidha kwa mabasi ya mjini, Mamlaka imetoa maelekezo yafuatayo:
  1. Kuhakiksha kuwa abiria wote wanapatiwa tiketi
  2. Kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa Sheria ikiwemo kutokamilisha safari maarufa kama kukata ruti, kubadili njia na unyanyasaji wa aina yoteyote kwa abiria
  3. Kutokutumia wapiga debe
  4. Wafanyakazi wa mabasi kuvaa sare nadhifu wakati wote.
Mamlaka ya SUMATRA inaendelea kuimarisha ushirikiano kwa kufanya kazi kwa karibu  na Mamlaka zingine kama Wakuu wa Mikoa, Serikali za Mitaa, Mamlaka za Miji, Polisi, TBS, TANROADS, Kamisheni ya Bima na wananchi kwa ujumla, katika kuleta mageuzi kamili ya utoaji wa huduma za usafiri wa barabara kwa kiwango cha juu.

A.S.K. Kilima
KAIMU MKURUGENZI MKUU
2 Aprili, 2013
 
 
 
 

Picha na mitandao mbalimbali

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO