Waumini wa dini ya Kiislamu wakibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', wakati wakiingiza jeneza hilo Msikiti wa Mwembeshauri, kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya kuelekea kijijini kwa marehemu, Kitumba Wilaya ya Kati kwa maziko, mchana huu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Ali Mohamed Shein, wakishiriki katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ramadhan Nasib 'Diamond Plutnum' (kulia), akiwa ni mmoja kati ya wasanii waliohudhuria katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri, mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja. TAARIFA HII NA PICHA NI KWA HISANI YA HAKINGOWI.COM
PICHA ZIFUATAZO ZINAONESHA NAMNA WANANCHI WA KAWAIDA, WADAU WA SANAA NA WASANII MBALIMBALI WAKISHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAZIKO YA BI KIDUDE. PICHA KUTOKA AUDIFACE JACKSON BLOG
Jeneza la bibi likielekea msikiti kwa ajili ya kusaliwa
Tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi R.I.P..........KIDUDE BINTI BARAKA
Mtangazaji Hassan Bond, Fid Q, Diamond Platnumz na Ruge Mutahaba wakiwa msibani nyumbani kwamarehemu bi Kidude, Zanzibar
Msanii Fid Q, Baraka cousin ya Marehemu Bi Kidude na Hassan Bond Mussa (FID Q ndo alikuwa msanii wa kwanza mkubwa kufika msibani kwa bibi)
Ruge mutahaba, Babu Tale and Guru. .......msibani kwa Bi Kidude
Guru G na Mh Bhaa mazikoni
Hassan na Fid Q wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya Marehemu Bi Kidude
Sehemu ya umati wa Watu waliofika msibani
0 maoni:
Post a Comment